loader
Serikali yapokea vifaa tiba vya milioni 864/- kutoka Misri

Serikali yapokea vifaa tiba vya milioni 864/- kutoka Misri

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa dawa pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya shilinigi milioni 864 vitavyosaidia katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali kutoka katika Serikali ya Misri.

Msaada huo umetolewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kupitia kwa Balozi Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abouelwafa na kupokelewa na katibu Mkuu Wizara ya Afya Profesa  Abel Makubi kwa niaba ya Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya.

Akipokea msaada huo, Profesa Makubi amesema, msaada huo umeletwa baada ya ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutembelea nchini Misri mnamo mwezi November mwaka jana 2021.

“Tunamshukuru sana Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania pamoja na Serikali ya Misri kwa kushirikiana na Tanzania hasa katika kuboresha Sekta ya Afya kwa kusaidia mahitaji mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.”amesema Profesa Makubi.

Aidha Profesa Makubi amesema msaada huo utaenda kuwasaidia wananchi wenye uhitaji katika vituo mbali mbali vya kutolea huduma za afya nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abouelwafa amesema kujitoa kwa Serikali ya Misri, kusaidia Sekta ya Afya ni kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi, ikiwemo kuboresha Sekta ya Afya nchini kwa kupambana dhidi ya magonjwa.

“Serikali ya Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusaidia Maendeleo ya Watanzania, hasa katika kuboresha Sekta ya Afya, hii inatokana na nia njema ya Mhe. Rais Samia katika kuleta maendeleo kwa wananchi, hususan katika kuboresha Sekta ya afya.” Amesema Mhe. Balozi Abouelwafa.

Kwa uongozi makini chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Misri imetoa ahadi kuendelea kusaidi Sekta ya Afya nchini kwa kuendelea kuleta Dawa pamoja na vifaa tiba kwaajili ya kupambana dhidi ya Magonjwa mbalimbali.

 

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a7d44ae0f94aaec7654c7ffb02797cf6.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi