loader
Wahandisi wanawake wasisitizwa kujisajili

Wahandisi wanawake wasisitizwa kujisajili

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi), imewataka wanafunzi wote wa kike kutoka vyuo mbalimbali wanaosomea fani zinazohusiana na Ujenzi kuweza kujisajili katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), ili kuingia katika mfumo maalumu wa kihandisi.

Hayo yameelezwa na Mhandisi Nancy Mduma kutoka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), wakati akifungua semina elekezi kwa wanafunzi wa kike kutoka chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST), kwenye ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara.

Mhandisi Mduma amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa wahandisi wanaomaliza vyuo kujisajili katika bodi hiyo kwani kuna kazi nyingine za kihandisi zinataka mhandisi aliyesajiliwa tu.

“Serikali sasa inalenga kuwawezesha wahandisi wanawake kufikia madaraja ya juu ya uhandisi, na hili kufikia madaraja hayo ni bora kila mhandisi baada ya kumaliza chuo aweze kujisajili na kuingia kwenye mfumo wa Bodi ya Wahandisi,” amesisitiza Mhandisi Nancy

Kwa upande wake Mratibu kutoka Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB), Mhandisi Victoria Haule amesema kuwa kazi kubwa ni kuwahamasisha Wanawake kushiriki katika kazi za Barabara ili kuongeza wigo mkubwa wa maendeleo unaofanywa na wanawake kutoka sehemu mbalimbali.

Aidha, katika mada nyingine zilizotolewa ni pamoja na kuangalia mchakato wa usajili kwa makampuni ya wanawake, kupitia mwongozo wa kuimarisha ushiriki wa wanawake katika kazi za barabara na masuala mtambuka. Zaidi ya wanachuo 70 wameweza kushiriki katika Uwasilishwaji wa mada mbalimbali zinazohusu kushiriki kazi za barabara.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a800502ecfeb297c556d312292a588a9.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi