loader
Mkurugenzi wa Kampuni ajitosa kiti cha Spika wa Bunge

Mkurugenzi wa Kampuni ajitosa kiti cha Spika wa Bunge

MWANASHERIA Andrew Kevela ambaye pia ni mkurugenzi wa Sheria kampuni ya Yono Auction Mart & Company amechukua fomu ya kuwania spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania lengo likiwa kuunga juhudi za Raisi Samia Suluhu Hassan kutaka vijana wajitokeza kuwania nafasi hiyo na wasikubali kutumiwa na wengine.

Akizungumza wakati wa kuchukua fomu hiyo makao makuu ya Chama Chama Mapinduzi (CCM)  Lumumba, alisema alipata nguvu ya kuchukua fomu hiyo baada ya kauli ya Rais aliyoitoa wakati akifunga kongamano la Vijana la kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru Zanzibar.

Alisema kupitia kauli hiyo ambayo ilikuwa ikimtambua kama kijana ndiyo wabunifu, vijana  ndiyo wabeba maoni aliona ni bora kutumia fulsa  hiyo katika kuwania nafasi hiyo kuliko kuwa nyuma ya watu wengine.

“Jambo la msingi lililonisababisha nije kuchukua fomu, kwamba Raisi alitaka vijana tusitumike kubeba watu na tujitokeze wenyewe katika kuwania kwakuwa yeye atakuwa nyuma yetu kuhakikisha anatulinda na haki inapatikana” alisema.

Uchukuaji fomu kupitia CCM ulianza unatarajia kukamilika Januari 15 mwaka huu, ambapo  Januari 17  Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho itakutana kwa ajili ya kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa wagombea waliojitokeza kuomba kiti cha uspika.

Nafasi ya Uspika ipo wazi baada ya aliyekuwa Spika Job Ndugai kujiuzulu baada ya kutoa kauli ya kupinga Serikali kukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kusababisha mjadala mitandaoni.

Mwisho.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c9e50a6df693172791614179dbe79552.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Mohamed Mussa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi