loader
Mjumbe Mkutano MKuu CCM Taifa, arejesha fomu ya uspika wa bunge

Mjumbe Mkutano MKuu CCM Taifa, arejesha fomu ya uspika wa bunge

Mjumbe wa Mkutano MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Wilaya ya Temeke, Mohamed Mmanga ambaye amejitosa katika nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jana Januari 14, 2022,  aerejesha fomu ya kugombea wa kiti hicho huku akiahidi kuliongoza vyema bunge hilo endapo atapewa nafasi.

Akizungumza baada ya kurudisha fomu hiyo katika ofisi ndogo ya chama Cha Mapinduzi Lumumba jijini Dar Es Salaam Mmanga alisema ameridhishwa na idadi kubwa ya waliojitokeza kuchukua fomu hiyo kwa kuwa inaonesha kukua kwa demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

"Hii ndiyo demokrasia ya kweli, siyo jambo la kawaida kuona idadi kubwa ya watu ikijitokeza kuwania kwa lengo la kuwania kiti hi hicho, nimeliacha suala la mchakato huo katika chama,naamini kila kitu kinakwenda vizuri" alisema Mmanga.

Hatua ya Mmanga na wanachama wengine wa chama hicho kujitokeza kuwania nafasi hiyo, imekuja siku chache baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Job Ndugai kujiuzulu nafasi yake na hivyo kufanya kiti hicho kuwa wazi.

Hadi jana idadi ya waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo kupitia Ofisi za Chama cha Mapinduzi(CCM) Makao Makuu Dodoma na Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba Dar es Salaam ni 66.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5027e72adc203d4d6a0dc2d9536451e1.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi