loader
Wasichana vinara Matokeo  kidato cha nne

Wasichana vinara Matokeo kidato cha nne

BARAZA LA Taifa la Mitihani (NECTA), limetangaza matokeo ya kidato cha nne huku wasichana wakiibuka vinara zaidi katika orodha ya wanafunzi 10 bora kitaifa.

Matokeo ya kidato cha nne haya hapa

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde wakati akitoa taarifa ya matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne amesema matokeo ya mwaka huu wasichana nane wameingia kwenye orodha ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne uliifanyika Novemba mwaka jana.

Kati ya hao, wasichana saba wanatoka shule ya St. Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya, msichana mwingine akitoka shule ya Bright Future Girls huku wavulana pekee walioingia kwenye 10  bora kitaifa wakitoka shule za Feza Boys ya Dar es Salaam na Ilboru ya Arusha.

Walioingia kwenye orodha hiyo ni pamoja na Consolata Lubuva, Buthoi Nkangaza, Wilihelmina Mujarifu, Glory Mbele na Mary Ngoso, wote kutoka shule ya St. Francis Girls iliyopo mkoani Mbeya.

Wengine ni Holly Lyimo (Bright Future Girls), Blandina Chiwawa (St. Francis Girls), Imam Mogaeka (Feza Boys), Mfaume Madili (Ilboru) na Clara Assenga (St. Francis Girls).

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi