loader
Uhamiaji walia utapeli mitandaoni, yataadharisha wananchi

Uhamiaji walia utapeli mitandaoni, yataadharisha wananchi

IDARA ya Uhamiaji imetadharisha wananchi juu ya utapeli  unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajira zinazotolewa na idara hiyo.

Taarifa ya Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Paul Mselle, imesema hivi karibuni Idara  hiyo  ilitangaza nafasi za ajira 470 za Cheo cha Konstebo wa Uhamiaji kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo magazeti, mitandao yake ya kijamii (Instagram, Twitter, Facebook) na tovuti.

“Kufuatia tangazo hilo kumekuwepo na taarifa zenye lengo la kuwalaghai wananchi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi yao kupigiwa simu au kupokea ujumbe kwa njia ya simu unaowataka kutuma fedha ili wasaidiwe kupata nafasi za ajira hizo.” amesema na kuongeza

“Idara inapenda kuufahamisha Umma kuwa mchakato wa ajira unaendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za ajira kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la ajira.

Aidha, amesema hakuna malipo yoyote yanayohitajika kwa ajili ya kupata nafasi za ajira za Uhamiaji na kuwataka wananchi kupuuza na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusu ujumbe wowote unaowataka kutuma kiasi chochote cha fedha ili waweze kupatiwa nafasi hizo.

Amesema taarifa rasmi za Idara, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo Vyombo vya Habari, tovuti ya Idara ambayo ni www.immigration.go.tz na mitandao ya kijamii.

Aidha, amesema Idara inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wanaojihusisha na uhalifu huo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e3ab7e353beed2f75075bb8f473470d2.png

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi