loader
TPA yajivunia ufanisi wa bandari zake  yaazimia kuzalisha Shi trilioni moja

TPA yajivunia ufanisi wa bandari zake yaazimia kuzalisha Shi trilioni moja

MAMLAKA ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ipo salama na utendaji wake unaridhisha kutokana na ufanisi mkubwa unaendelea kupatikana katika bandari zote, anasema Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Eric Hamissi.

Mkurugenzi huyo anasema hayo akikanusha taarifa za uzushi zinazosambazwa na watu wasioitakia mema TPA wanaodai  kushuka kwa mapato ya TPA.

Huku akitaja takwimu zinazothibitisha mafanikio ya TPA katika kipindi cha miezi sita iliyopita, Mkurugenzi Mkuu Hamissi  anasema hadi kufikia Desemba 31, 2021, TPA ilihudumia meli 2,325 ambazo ni asilimia 62.8 ya lengo la mwaka mzima la kuhudumia meli 3,704.

 

Pia anasema hadi kufikia Desemba 31, 2021, TPA ilihudumia magari 101,692 ambayo ni sawa na asilimia 101.7 ya lengo liliwekwa la kuhudumia magari 100,000 kwa kipindi hicho.

 

Aidha anasema hadi kufikia Desemba 31, 2021, TPA ilihudumia tani milioni 9.895 za shehena mbalimbali sawa na asilimia 107.7 ya lengo la kuhudumia tani milioni 9.190; ikiwa ni sawa na asilimia 54.5 ya lengo la kuhudumia tani milioni 18.2 kwa Mwaka mzima.

Mkurugenzi huyo katika mazungumzo anasema mabadiliko makubwa yanayofanyika kupitia Mradi wa DMGP unaoendelea kutekelezwa katika Bandari ya Dar Es Salaam wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 421 kumeinua uwezo wa bandari hiyo na ukikamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa TPA.

Pamoja na kusema kwamba Menejimenti yake itasimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa kuzingatia thamani halisi ya uwekezaji huo, Mkurugenzi Mkuu Hamissi anasema tayari manufaa yake yameshaanza kuonekana.

Mradi huo unatekelezwa kwa Fedha kutoka vyanzo vitatu ambavyo ni Mkopo wa dola za Kimarekani milioni 345 kutoka Benki ya Dunia; Msaada (grant) Dola za Kimarekani milioni 12 kutoka DFID; na Mapato ya ndani ya TPA ya dola za Kimarekani Milioni Sitini na Nne (64) umeifanya Bandari ya Dar es salaam kuwa na shughuli nyingi za kuhudumia meli na shehena.

Anasema wakati hadi kufikia Desemba 31, 2021, TPA ilikusanya Sh bilioni 508.618 sawa na asilimia 90.61 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 1.1 kwa Mwaka wa Fedha 20211/2022 kwa mabadiliko yanayoendelea kuwezeshwa na mradi huo hadi kufikia Desemba 31, 2021, TPA ilihudumia makasha TEUS 383,978 sawa na asilimia 97.3 ya lengo la kuhudumia makasha TEUS 394,662 hii ikiwa ni sawa na asilimia 97.3 ya lengo lililowekwa kwa kipindi hicho.

Kukamilika kwa mradi huu mwezi Juni,2024 kutaiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena ya tani milioni 25 kutoka tani milioni 16 za sasa.

Aidha, Bandari ya Dar es Salaam itaweza kuhudumia meli zenye urefu wa mita 303 na zenye kubeba makasha mpaka TEUS 8,000 na kuwa moja kati ya bandari zenye uwezo na ufanisi mkubwa katika pwani ya Afrika Mashariki.

Anasema kukukubalika kwa Bandari ya Dar es salaam katika utoaji wa huduma na pia tozo zake kumefanya kwa sasa kuwepo na meli nyingi zinazosubiri kuingia bandarini.

 

Hali hii ya ongezeko kubwa la shehena zinazoingia nchini kutokana na juhudi zinazofanywa za Serikali ya Awamu ya Sita kuvutia biashara na uwekezaji nchini.

“TPA tumejipanga kuongeza uwezo wetu wa kiutendaji ili kukabiliana na ongezeko hilo ikiwa ni pamoja na kuhudumia meli hizo kwa muda mfupi iwezekanavyo na kuendelea kuzifanya Bandari za TPA kuwa chaguo la kwanza kwa Wasafirishaji wa bidhaa za Tanzania na Nchi jirani” anasema Mkurugenzi Mkuu Hamissi.

Naye Mkurugenzi wa Bandari ya Dar Es Salaam Mhandisi Juma Kijavara anasema, watumishi wa Bandari ya Dar es salaam wamejipanga kufanya kazi kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa bandari hiyo inaendelea kuwa kinara wa kuingiza mapato katika Mamlaka ya Bandari Tanzania.

“Tutafanya kila linalowezekana na kujituma ili kuiwezesha TPA kufikia lengo la kuzalisha Shilingi trilioni moja katika mwaka wa Fedha 2021/ 2022” anasema Kijavara.

Aidha, Kijavara amehimiza utendaji unaozingatia uadilifu na kuahidi kutoa motisha kwa watumishi wa Idara na vitengo vyote watakaofanya kazi na kuvuka malengo yaliyowekwa ili kukabiliana na kasi ya ongezeko la shehena bandarini.

Mwenyekiti wa DOWUTA Taifa, Mwalami Manyara anasema bandari kama lango la nchi nan chi jirani  inatakiwa kuwa na uwajibikaji mkubwa ili kuwezesha uchumi wa taifa na wan chi jirani.

Pia mwenyekiti huyo anasema Serikali inastahili pongezi kwa kuboresha Huduma za bandari nchini.

“Katika kipindi kifupi, Mheshimiwa Rais amefanya maamuzi muhimu ya kuongeza Ufanisi katika Mamlaka hii kwa kuweka uongozi mpya, kutoa maelekezo ya kuboresha utendaji kazi, kutoa fedha Shilingi bilioni 210 za kununulia vifaa vya utendaji kazi na kutoa miongozo ya kuhakikisha bandari zote zinafanya kazi kikamilifu katika nyakati zote za mwaka,” anasema.

Mkurugenzi TPA, Hamissi kwa upande wake amewataka Watumishi wote wa TPA kufanya kazi kwa weledi na moyo wa uzalendo ili kutimiza majukumu yao kwa wakati na kwa viwango vya juu kabisa vya ubora.

Anasema ni wajibu wao kuhakikisha kwamba uwekezaji mkubwa unaofanywa katika Sekta ya Bandari unajibu kwa kuwa bora katika kila kidara na kujituma kwa weledi na uzalendo ikiwa na pamoja na kuendeleza kazi zilizoasisiwa na awamu zilizotangulia.

Anasema TPA inaendelea na maboresho mbalimbali ya miundombinu nchini katika bandari mbalimbali kwalengo la kuongeza ufanisi.

Bandari kuu tatu za Dar es salaam , Tanga na Mtwara zimekuwa katika maboresho mbalimbali.

Mradi wa ujenzi wa gati jipya bandari ya  mtwara uliochukua miezi 22 hadi kukamilika kwake na kutumia  Sh bilioni 157.8  umeipaa hadhi mpya bandari hiyo ambayo ni ya siku nyingi  huku ukiongeza uwezo wa Bandari hiyo  kutoka kusafirisha tani laki 4 mpaka zaidi ya tani milioni 1 za mizigo kwa mwaka.
Nayo Bandari ya Tanga ambayo ni miongoni mwa bandari ambapo serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa ikiwemo ujenzi wa gati mpya yenye urefu wa meta 450 sambamba na ,uboreshaji wa vifaa kwa ajili ya kupakulia shehena ya mizigo, ujenzi wa gati awamu ya kwanza ya meta 300 bado unaendelea na upo katika hatua nzuri  ya kukamilisha  meta 150 za makubaliano ya awali.

Mnamo Novemba mwaka jana bandari  hiyo iliweza kupokea vifaa kwa ajili ya kuimarisha utendajikazi na hivyo kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo kutoka tani 750,000 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni tatu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7249a5980472c1db002b755dbd837593.jpg

OPERESHENI ya kuondoa wazururaji na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi