loader
Uganda yaafiki kuongeza maofisa wa afya mpakani

Uganda yaafiki kuongeza maofisa wa afya mpakani

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya maofi sa wa afya katika vituo vya mpakani na Kenya vya Busia na Malaba kutoka 50 hadi 100, kama sehemu ya juhudi za kuondoa mrundikano wa malori kwenye vituo vya mpakani.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotumwa kwa HabariLEO kutoka Idara ya Mawasiliano na Masuala ya Umma katika Sekretarieti ya EAC, Kenya imeufahamisha Mkutano wa Tatu wa Pamoja wa Sekta Mbalimbali wa Mawaziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Afya na Uchukuzi uliofanyika Ijumaa kuhusu upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kupima Covid-19 na wafanyakazi wake kusaidia Uganda katika upimaji wa Covid-19 kwenye vituo vya mpaka.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya, Adan Mohamed, Kenya ilithibitisha kuwa tayari kupeleka haraka wafanyakazi 15 au zaidi wa afya na kutoa vifaa ili kuboresha upimaji wa Covid-19 katika vituo vya mpakani vya Malaba na Busia.

Uganda ilikubali kutambua cheti cha kipimo cha Covid-19 kitakachotolewa na Wizara ya Afya ya Kenya kwa muda wa saa 72 kwa kutumia itifaki za upimaji. Kwa upande wake, Mohamed alisisitiza haja ya kupunguza ucheleweshaji wa kiutawala ili kuongeza uondoaji wa haraka wa mrundikano uliopo kwenye mipaka ya Malaba na Busia.

Walibainisha mwenendo wa sasa wa kuwaondoa madereva wa malori katika vituo hivyo vya mpaka hautoshi kuondoa mrundikano uliopo wa malori. Mawaziri waliipongeza Serikali ya Uganda kwa hatua iliyofikiwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa Januari 10, mwaka huu na kuitaka Uganda kuongeza uwezo wake wa kuwapima madereva wa malori ili kurahisisha uondoaji wa haraka wa bidhaa.

Mkutano huo ulihimiza Jamhuri ya Kenya kuunga mkono mchakato huo kwa kutoa nguvu kazi ya ziada na vifaa ili kuharakisha mchakato wa upimaji na utoaji wa vibali. Mawaziri waliiagiza sekretarieti kuitisha mkutano wa ufuatiliaji wa mawaziri/Katibu wa Wizara ya Afya ili kujadili suluhisho la muda mrefu ili kurahisisha harakati za kuvuka mpaka.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/41f44651a92f59fd23ace776ed6199f3.jpeg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi