loader
Mchakato wa ajira EAC warejea

Mchakato wa ajira EAC warejea

MCHAKATO wa ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umerejea baada ya walioitwa katika usaili kupangiwa upya usaili jana Januari 17 hadi Februari 2, mwaka huu.

Waombaji wa nafasi mbalimbali za kazi katika EAC watafanya usaili katika mkutano kwa njia ya mtandao katika wizara zinazohusika na masuala ya EAC katika nchi wanachama watakapokwenda na vyeti vyao halisi. Taarifa iliyotolewa na Sekretarieti ya EAC kwa umma inaonesha majina ya waombaji wanaoitwa katika usaili, tarehe za kufanya usaili na eneo husika la usaili katika makundi tofauti.

Takribani nafasi 49 za ajira katika EAC zilitangazwa ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi.

Hata hivyo, baadaye mchakato huo uliingia dosari kwa kupingwa na baadhi ya nchi baada ya kutolewa kwa majina ya walioitwa kwa ajili ya usaili hali iliyolazimu kusitishwa kwa muda kwa mchakato huo.

Baadaye Baraza la Mawaziri la EAC lilitangaza kuendelea kwa mchakato wa ajira katika nafasi zilizositishwa Oktoba mwaka jana huku wakitaka baadhi ya nafasi za ajira kutangazwa upya. Walieleza kuwa ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ajira kwa nchi wanachama, nafasi 11 za kazi zitatengwa kwa ajili ya Sudan Kusini.

Mchakato huo ulielezwa kuendelea mwezi huu, lakini baraza limeitaka sekretarieti kutangaza upya nafasi ambazo walioitwa kwenye usaili walitoka nchi moja mwanachama pamoja na kutangaza upya nafasi ambazo mtu mmoja ndiye pekee aliyeitwa kwa ajili ya usaili.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya, Adan Mohamed alisema waombaji walioteuliwa kutoka nchi wanachama wa EAC watapokea mialiko kutoka sekretarieti kushiriki katika usaili huo.

Mohamed alisema baraza katika majadiliano yake lilibaini kuwa mchakato wa kuajiri ulikuwa na baadhi ya kasoro na ili kuhakikisha usawa kati ya nchi wanachama katika mchakato wa kuajiri, nafasi 11 kati ya nafasi zilizokuwa wazi zitatengwa kwa ajili ya Sudan Kusini.

Hii ni kwa mujibu wa agizo la Baraza Namba 41 kwa Sekretarieti kuhakikisha Sudan Kusini inapata nafasi 11 kati ya 15 ambazo hazijaorodheshwa katika mchakato wa kuajiri EAC. Baraza la Mawaziri liliiagiza sekretarieti kutangaza tena nafasi tatu za Uganda, ambazo ni Mhariri wa Kumbukumbu Rasmi za Bunge (Hansard); Mwandishi wa Hansard na Karani Msaidizi Mwandamizi.

Kikao hicho kilibaini kuwa kulikuwa na makosa katika matangazo ya nafasi tatu zilizowaondoa wagombea kutoka Uganda na kupendekeza sekretarieti kutangaza upya nafasi hizo. Mawaziri walibaini kuwa kwa nafasi ambazo ni wagombea kutoka nchi moja washirika pekee ndio wameorodheshwa, zilitakiwa kupitiwa upya kwa nia ya kuhakikisha inatoa fursa ya ushindani.

Mkutano huo pia ulibainisha kuwa baadhi ya matangazo yalikuwa na vikwazo vingi na yalihitaji uhakiki ili kuwezesha watahiniwa wengi kutuma maombi ya kazi hizo. Mkutano huo ulibainisha kuwa si sahihi kwa nafasi yoyote kupata mgombea mmoja pekee anayekidhi matakwa.

Mawaziri waliiagiza sekretarieti kuendelea na kazi za kuajiri katika nafasi zote ambazo hazikutolewa maagizo kuanzia Januari 2022 na kusisitiza kuwa Burundi itapewa kipaumbele katika uajiri katika awamu ijayo ya kuajiri kwa mujibu wa maagizo ya Kikao cha 39 cha Baraza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d28f64a77ebf439bbe572512fabb9cef.jpeg

Kiongozi wa Azimio la Umoja ...

foto
Mwandishi: Na Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi