loader
Aliyeokoa watu 1,200 akutwa na hatia ya ugaidi

Aliyeokoa watu 1,200 akutwa na hatia ya ugaidi

SHUJAA wa “Hotel Rwanda” ameshindwa kufi ka katika Mahakama ya Kigali Jumatatu huku waendesha mashtaka wa serikali wakitaka kumuongezea kifungo kwa tuhuma za ugaidi kutoka miaka 25 hadi maisha.

Jaji aliahirisha kesi hadi Jumanne baada ya Paul Rusesabagina (67), mkosoaji mkubwa wa serikali ambaye vitendo vyake wakati wa mauaji ya halaiki ya 1994 nchini Rwanda vilichochea filamu kali ya Hollywood, kukataa kuhudhuria kesi hiyo.

Rusesabagina na washitakiwa wenzake 20 walitiwa hatiani na kuhukumiwa mwezi Septemba kwa kuunga mkono kundi la waasi wenye silaha katika kesi ambayo makundi ya kutetea haki za binadamu na wafuasi wake walidai kuwa ni uongo. Hata hivyo, waendesha mashitaka walitaka kifungo cha maisha jela na kukata rufaa, wakisema adhabu hiyo ni ndogo kwa meneja huyo wa zamani wa hoteli.

Washtakiwa wenzake wote walifikishwa mahakamani Jumatatu wakiwa wamevalia sare za pinki zinazovaliwa na wafungwa wa nchini hapa. Mmoja wa mawakili wao, Jean Rugeyo, alidai taratibu hazikufuatwa hivyo basi kesi hiyo iahirishwe kwa ajili ya washtakiwa wote.

Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Bonaventure Ruberwa, alidai Rusesabagina ambaye amekuwa akishikiliwa gerezani tangu kukamatwa kwake Agosti 2020, alikuwa ameitwa kihalali kufika mahakamani. “Alikataa kwa makusudi kutia saini barua hiyo na pia alikataa kuhudhuria kikao.

Hili lisicheleweshe kusikilizwa,” alisema. Jaji Francois Regis Rukundakuvuga alisema uamuzi utatolewa Jumanne kuhusu kuendelea na rufaa hiyo iwapo Rusesabagina hayupo. Familia yake ilisema wiki iliyopita kwamba Rusesabagina hatashiriki “katika rufaa iliyowasilishwa ya mfungwa wa kisiasa” na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Rwanda kumwachilia baba yao.

“Inaendelea kuonesha kuwa huu si mchakato wa kisheria, lakini ni mchakato unaoendelea wa kisiasa wa kuaibisha na kukashifu mkosoaji wa haki za binadamu wa utawala,” familia ilisema katika taarifa yake Ijumaa. Rusesabagina alikuwa Mnyarwanda maarufu zaidi kimataifa baada ya mwigizaji wa Marekani, Don Cheadle kuigiza matendo yake wakati wa mauaji ya kimbari katika filamu ya mwaka 2004 ya “Hotel Rwanda”.

Alikamatwa wakati ndege aliyoamini ilikuwa ikielekea Burundi ilipotua badala yake mjini Kigali katika tukio ambalo familia yake imeele

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b1b63244d14451e6d5cb9231fb8372d4.png

Kiongozi wa Azimio la Umoja ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi