loader
Sehemu kubwa Dar kupata mabasi mwendo kasi

Sehemu kubwa Dar kupata mabasi mwendo kasi

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi yaendayo haraka (DART) umesema ifi kapo mwaka 2026 sehemu kubwa ya mkoa wa Dar es Salaam itakuwa imeungwanishwa na mfumo wa barabara zake na hivyo kufanya huduma za mabasi yaendayo haraka kutoa huduma katika maeneo hayo.

Aidha ili kuondoa adha ya mlundikano wa abiria katika vituo vyake, Dart inatarajiwa kufunga mfumo wa uongozaji mabasi ujulikanao kama ‘Interegence Transport System (ITS) ambao humwezesha msimamizi kuwasiliana moja kwa moja na dereva inapotokea basi limechelewa katika kituo.

Hayo yamebainishwa katika warsha ya siku moja baina ya wakala, wahariri pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali. Akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu , Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Dart, Frank Kalugendo, alisema mtandao huo wa miundombinu ya mabasi unahusisha awamu sita za ujenzi.

Awamu ya kwanza ni Kimara hadi Kivukoni yenye kilometa 20.9 na tawi kutoka Magomeni kwenda Morocco pamoja na Fire kwenda Kariakoo ambako huduma zinaendelea.

Alisema awamu ya pili inatoka ‘City Centre’ kwenda Mbagala Rangi tatu pamoja na tawi la kutoka JKT Mgulani kwenda Magomeni ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 45 upande wa barabara huku ujenzi wa vituo ukiendelea Kuhusu awamu tatu, ujenzi wa miundombinu utahusisha barabara kutoka mjini hadi Gongo la Mboto ikiwa na tawi litakaloanzia Tazara kwenda Buguruni hadi Kariakoo kupitia barabara ya Uhuru ambayo usanifu wake umekamilika.

“Tumefanya mchakato wa kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo, tumeshapata kibali cha Benki ya Dunia kwa ajili ya kumwajiri mkandarasi na kwa sasa tunasubiri ukamilishaji wa mkataba kutoka kwa Mwanasheria wa Serikali na wakati wowote mwaka huu ujenzi wake utaanza,” alisema.

Alisema awamu ya nne itahusisha ujenzi wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Maktaba hadi Dawasa Boko huku. Awamu ya tano itahusisha ujenzi wa wa Barabaraya Mandela kuanzia Daraja la Ubungo hadi Daraja la Nyerere Kigamboni na barabara kuanzia Tabata Segerea hadi njia panda ya Kigogo ambazo zote usanifu wake na majadiliano yanaendelea na wafadhili ili kupata fedha za ujenzi.

Alisema awamu ya sita itahusisha ujenzi wa barabara ndogo za kuingia zitakazounganisha barabara mbalimbali na mipango yote inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2030. Akizungumzia mfumo wa usimamizi wa mabasi hayo kwa lengo la kupunguza msongamano au abiria kukaa muda mrefu vituoni, Meneja wa Tehama wa Dart, Ngwanashigi Gagaga alisema matarajio ni kwamba, ifikapo mwisho wa mwaka huu utakuwa umefungwa kwa lengo la kuondoa adha hiyo.

Alisema hatua hiyo mbali na uboreshaji wa huduma za ukataji wa tiketi kwa kutumia mfumo wa kisasa wa mashine za Poss, umelenga kuhakikisha huduma zinazotolewa na wakala zinakuwa bora kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Dart, Edwin Mhede alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya wakala huyo na wadau mbalimbali hususani vyombo vya habari katika masuala yote yanayohusisha utoaji huduma. Alisema hatua hiyo itaondoa changamoto zinazojitokeza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/99628c9667cc9114cd7ac512a1ab9531.jpeg

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Na Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi