loader
Ndumbaro kukutana wadau wa uwindaji kitalii

Ndumbaro kukutana wadau wa uwindaji kitalii

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ameahidi kukutana na wadau wa uwindaji wa kitalii wanaomiliki vitalu vya uwindaji nchini ambao si wanachama wa Chama cha Uwindaji wa Kitalii Tanzania  (TAHOA), mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Las Vegas Nevada, Marekani wakati  akitoa wito kwa kamati ya watu 10 aliyoiounda kwa ajili ya kumshauri namna bora ya kuendesha sekta ya uwindaji ya kitalii, kuwasilisha ripoti itakayomsaidia kuboresha minada ya kielektroniki ya biashara hiyo inayofuata hapo baadaye.

Ndumbaro alisema kuwa mkutano huo utakuwa na lengo la kuboresha mazingira ya biashara ya sekta hiyo ikiwemo uzoefu waliopata katika ushiriki wa maonesho ya 50 ya mwaka ya uwindaji wa kitalii yanayoendelea yakiwakutanisha watunga sera na wafanya uamuzi kutoka nchi mbalimbali duniani juu ya kuendeleza sekta ya uwindaji.

Aliwataka wadau wanaomiliki vitalu vya uwindaji wa kitalii nchini kuacha kulalamika badala yake wawasilishe ripoti hiyo ya ushauri kwa kuonesha waliyokubaliana kwa pamoja na waliyotofautiana aifanyie kazi.

Ndumbaro alisema kitendo cha kamati hiyo kushindwa kuwasilisha ripoti hiyo kwa wakati kumemfanya kuwa na wakati mgumu na kushindwa kufanya uamuzi wenye maslahi mapana pande zote mbili kwa maana ya serikali na wadau wa sekta hiyo.

Waziri Ndumbaro aliunda kamati ya watu 10 Juni 23, 2021 jijini Dodoma  ikiwa na watu  watano kutoka sekta binafsi na wengine  watano kutoka serikalini lakini mpaka sasa wameshindwa  kuwasilisha ripoti ya  ushauri.

Ndumbaro alisema kuwasilishwa kwa ripoti hiyo mapema  kutatoa mwelekeo wa namna bora ya kuendesha minada ya kielektroniki ya uwindaji wa kitalii inayofuata katika mazingira bora zaidi.

“Baadhi yenu mmekuwa mkilalamika tu kuwa hamtaki minada ya kielektroniki ya vitalu vya uwindaji wa kitalii, leteni ushauri kupitia ripoti hiyo  mkionesha sababu na njia mbadala kama serikali nini tufanye,”  alisema.

Kutokana na hali hiyo, Ndumbaro alisisitiza wadau hao waliopo Marekani ambao ni washiriki wa maonesho hayo 50, kiwasilisha ripoti mapema iwezekanavyo ili mwanzoni mwa mwezi ujao aitishe mkutano wa wadau hao.

Katika hatua nyingine, aliwapongeza wadau hao kwa maoni mazuri waliyotoa katika kikao alichofanya nao nchini humo.

Mwenyekiti wa Tahoa, Michel Matheakis alimshukuru Waziri Ndumbaro kwa kuwa muumini wa mazungumzo na kuahidi kuwa ripoti hiyo itawasilishwa ifanyiwe kazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/18f2299227c363c8980dee4dddb77144.jpg

BAADHI ya wanaume katika Kijiji cha Ikondamoyo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Marekani 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi