loader
Tuiunge mkono serikali utekelezaji miradi-Zitto

Tuiunge mkono serikali utekelezaji miradi-Zitto

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amewata viongozi na wanachama wa chama hicho kuunga mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayotekelezwa na serikali.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo la Kigoma Mjini uliofanyika Mjini Kigoma jana, Zitto  alisema kuwa chama hicho kinaunga kwa dhati utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayofanywa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo una faida ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi wa kawaida na kwamba hakuna sababu yoyote kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kupinga mpango huo.

 “Kwa sasa habari na hasira za uchaguzi mkuu uliopita ondoeni badala yake tuiunge mkono serikali katika utekelezaji wa miradi badala ya kupinga na hasa hapa mzingatie miradi yenye maslahi kwa maendeleo ya mji wa Kigoma Ujiji, lakini pia fuatilieni ahadi za miradi na utekelezaji wa miradi ambayo fedha zake zimepitishwa na serikali,"alisema Zitto.

Pamoja na hilo aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho mkoani Kigoma na nchini kote kwa jumla kuhoji viongozi wa maeneo yao sababu za miradi iliyopitishwa kutotekelezwa.

Akizungumzia mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kujiandaa  kwa kazi kubwa ya kushinda huku akihimiza kuundwa kwa tume uhuru ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi huo pamoja na kusimamia mchakato wa katiba mpya.

Mwenyekiti wa ngome ya vijana ACT Taifa, Abdul Nondo aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho kupiga kelele kuhusu utekelezaji wa miradi ambayo haijakamilika licha ya kuwepo kwa taarifa ya kutolewa kwa fedha za miradi.

Alitoa  mfano wa machinjio ya kisasa Kitongoni, Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao Shirika la Umoja wa Mataifa la Uwekezaji na Mitaji (UNCDF) limeshatoa Sh milioni 186 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo lakini Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imeshindwa kutoa Sh  milioni 14 kukamilisha mradi huo kwa miaka miwili sasa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/543e74397f730f3e5430bf3d20681c8b.jpg

MBUNGE wa Kigamboni, Dk Fausitine Ndugulile (CCM) ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi