loader
Nabi: Tunawaheshimu  Polisi Tanzania

Nabi: Tunawaheshimu  Polisi Tanzania

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema anawaheshimu wapinzani wake Polisi Tanzania kwa kujua ni miongoni mwa timu nzuri zinazosumbua akiamini  mchezo wa leo watakaokutana katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  hautakuwa rahisi.

Akizungumzia mchezo huo jana, Nabi alisema Polisi ni timu nzuri na imekuwa katika mwenendo mzuri, anaiheshimu na ndio maana waliwahi mkoani humo kujiandaa.

Mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, hawakupumzika na kuamua kwenda Arusha tangu Jumatatu ili kuzoea hali ya hewa na kujiweka imara kwa ajili ya mchezo na Polisi Tanzania.

“Polisi ni timu nzuri, inasumbua timu kuanzia mwanzo wa ligi na wako katika nafasi nzuri. Lakini sisi tumejipanga tukijua umuhimu wa mechi hiyo na lengo ni kupata pointi tatu,”alisema.

Yanga ikiwa Arusha kwa wiki moja ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya First Division Mbuni FC, ambapo alipanga asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwa hawapati namba katika michezo iliyopita na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Nabi alisema mchezo huo ulikuwa na lengo la kuhakikisha wanajenga utimamu wa mwili kwa wachezaji wote kujiandaa na Polisi Tanzania.

Yanga na Polisi zinatofautiana pointi 14 mmoja akiongoza kwa pointi 32 na mwingine akiwa na pointi 18 akiwa ndani ya tano bora za juu, kila mmoja akiwa amecheza michezo 12.

Ila vinara hao hawajapoteza mchezo wowote ikionesha dhahiri kuwa na safu bora ya ulinzi na hata kwenye ushambuliaji wako vizuri wakiwa wamefunga mabao 22 ndio timu inaongoza kwa magoli mengi.

Kwa upande wa Polisi sio wabaya wala sio wazuri, katika michezo mitano iliyopita wameonesha ni wagumu kupoteza, wameshinda mchezo mmoja na kupata sare nne.

Msimu uliopita Yanga iliondoka na pointi nne dhidi ya Polisi Tanzania ikipata ushindi wa bao 1-0 nyumbani kisha sare ya bao 1-1 ugenini.

Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania George Mketo alisema wamejipanga vizuri kushinda mchezo huo.

Alisema wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita anaamini hayatajirudia  kwakuwa ni muhimu kupambana na kupata pointi tatu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/027eb34e8b1f5669e1beb5675d874ce9.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi