loader
Serikali  kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi

Serikali kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amesema Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia zinazowakabili baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

Dk Gwajima ametoa kauli hiyo leo Januari 23, 2022 wakati akizindua Dawati la Jinsia kufuatia utekelezaji wa mradi wa kutetea haki za Jinsia unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). 

"Kuna matukio mengi ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii ikiwemo Vyuoni na shuleni hivyo kuna haja ya kuweka mikakati madhubuti ya kuanzisha Madawati ya Jinsia yanayofanya kazi kwa  mfumo wa kupima ufanisi wake ili isije ikawa tumefungua kwa mazoea yakakosa tija" amesema. Dk Gwajima.

Aidha, Dk Gwajima amesema Serikali imetekeleza mambo mengi katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kukuza uelewa wa wananchi kutoa taarifa za matukio, kuunda madawati ya jinsia 420 kwenye vituo vya polisi na 153 kwenye jeshi la magereza, Kamati 18,186 za Ulinzi wa Wanawake na Watoto zimeanzishwa nchini, Vituo vya huduma kwa wahanga vimeanzishwa kwenye hospitali 14, Sheria ya msaada kwa wahanga na 1 ya mwaka 2017 imetungwa.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga, amesema kuwa mradi wa ‘03plus’ utanufaisha Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Serikali ya awamu ya sita imejipanga kikamilifu kuondoa changamoto ya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwakilishi wa UNESCO nchini Tirso Santos amesema kwamba lengo la kuleta mradi huo ni kuona wanafunzi wa kike waliopo vyuo vikuu wakisoam kwa kujiamini

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/09b055f5d4892c16f9c1415d04c5180f.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi