loader
Ugawaji vitalu  kwa mnada  waingiza bil 19.2/-

Ugawaji vitalu kwa mnada waingiza bil 19.2/-

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema serikali imepata faida kubwa kutokana na matumizi ya mfumo wa ugawaji vitalu vya uwindaji kwa njia ya mnada ulioanza mwaka 2019, ambapo imepata Sh bilioni 19.2 ikilinganishwa na Sh bilioni 5.24 ambayo ingepatikana kama ingetumia njia ya zamani ya zabuni.

Aidha, alisema tangu mwaka 2019, hadi sasa jumla ya minada sita ya vitalu vya uwindaji wa kitalii imefanyika kwa njia ya mtandao. Masanja aliyasema hayo jana mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada wa sita uliofanyika kuanzia Januari 12 hadi 18, 2022.

Alisema katika mnada huo uliohusisha jumla ya vitalu 75 vya uwindaji wa kitalii, vitalu 49 umiliki wake unamalizika Desemba 31, 2022 huku vitalu 26 vikiwa wazi.

“Katika mnada huo, jumla ya kampuni 39 zilishiriki mnada na kampuni 26 kati ya hizo sawa na asilimia 54.2 zilishinda vitalu vya uwindaji 45,” alisema.

Katika mnada wa sita Sh bilioni 14.32 zilikusanywa ambapo Sh milioni 392.7 zilitokana na ada ya maombi ya ushiriki na Sh bilioni 13.86 zilitokana na ada ya vitalu.

Aliongeza kuwa ugawaji wa vitalu kwa njia ya mnada umewezesha nguvu ya soko kuonesha thamani halisi ya rasilimali muhimu ya nchi ya vitalu vya uwindaji kitalii.

“Kwa mfano kitalu kimoja daraja la tatu ambacho kilikuwa kiuzwe kwa njia ya zabuni shilingi milioni 41.58 kimeuzwa milioni 462 ambayo ni mara 11ya bei ya zabuni. Daraja la pili kilikuwa kiuzwe shilingi milioni 69.3 sasa kimeuzwa shilingi milioni 577.5 na daraja la kwanza shilingi milioni 138.6 lakini kimeuzwa shilingi milioni 658.3 kwa njia ya mnada,” alifafanua.

Alisema minada ya vitalu vingine vilivyobaki utafanyika Machi 2022 ambapo aliwaalika wadau wote wa utalii wanaopenda kujishughulisha na uwindaji wa kitalii kushiriki mnada huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e2e67e443f03bc6d685a8a2f20616dba.jpeg

BAADHI ya wanaume katika Kijiji cha Ikondamoyo ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi