loader
Tamisemi yapiga marufuku tozo kwa wajawazito

Tamisemi yapiga marufuku tozo kwa wajawazito

KATIBU Mkuu Ofi si ya Rais-Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa mkoani Njombe kusitisha malipo ya Sh 5,000 kwa wanawake wanaosubiri kujifungua katika magengo ya halmashauri hiyo maarufu kama mabweni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Nteghenjwa Hosseah imebainisha uamuzi wa Profesa Shemdoe wa kusitisha tozo hiyo ni kutokana na ukweli kuwa ni kitendo kinyume na mwongozo wa utoaji huduma za mama na mtoto.

“Kutokana na maazimio hayo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –Tamisemi amemwelekeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kusitisha mara moja malipo hayo na kuendelea kutoa huduma za mama na mtoto kwa mujibu wa Sheria na miongozo ya serikali,”alisema.

Aidha, Profesa Shemdoe amezikumbusha halmashauri zote nchini kuwa masuala yote yanayohusu huduma za afya yafuate sheria, kanuni na miongozi ya serikali.

Pia aliyataka mabaraza ya madiwani ya halmashauri zote nchini kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/765e35f81c8145a2ced18cbff8db2e5c.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi