loader
Serikali kushughulika na wanaopandisha bei bidhaa

Serikali kushughulika na wanaopandisha bei bidhaa

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk, Ashatu Kijaji amesema Serikali haitavumilia tabia ya baadhi ya  wafanyabiashara wenye dhamira ovu ya kuwaumiza wananchi kwa kujiamulia kupandisha bei za bidhaa bila kufuata utaratibu.

Dk Kijaji amelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya uchunguzi uliofanywa na Tume ya Ushindani ( FCC) kuhusu uhaba na kupanda kwa bei za vinywaji baridi uliotokea Oktoba hadi Januari 2022.

Akizungumza Januari 23,2022 mkoani Shinyanga, Dk Kijaji amesema Serikali inajukumu la kusimamia ushindani wa haki kwenye soko kwa kudhibiti mienendo hadaifu au kandamizi ya wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara wanaopandisha holela wa bei za bidhaa. 

Aidha, Waziri kijaji aliwahakikishia watanzania kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa Sukari hiyo ya viwandani inapatikana kwani hadi sasa tani 25,000 ya sukari ya viwandani imeingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam na inaendelea kupokelewa kwa kuwa Sukari hiyo kwa sasa inasafirishwa kwa njia ya mbadala ya ufungashaji shehena usiotumia makasha (containers), yaani break-bulk.

Akielezea hatua nyingine ambazo Serikali imechukua ili kutatua changamoto hiyo, Waziri Kijaji amezielekeza Mamlaka na Taasisi za Serikali zikiongozwa na Tume ya Ushindahi (FCC) zilizopewa dhamana ya kusimamia mienendo ya masoko ya bidhaa kutekeleza wajibu huo kikamilifu na kwa umakini mkubwa ili kudhibiti mienendo hadaifu au kandamizi ya wazalishaji wa bidhaa na wafanyabiashara kwenye soko ikiwa ni pamoja na upandishaji holela wa bei za bidhaa nchini.

Aidha, Waziri Kijazi amewaelekeza Maafisa Biashara wa Mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, kupitia Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/61c69a4e25912883e8d61f2ee425c619.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi