loader
Doris Moller, ElementsClub wakabidhi vifaa tiba hospitali ya palestina

Doris Moller, ElementsClub wakabidhi vifaa tiba hospitali ya palestina

TAASISI ya Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na Elements Club na wasanii wa bongo fleva, imekabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali katika hospitali ya Palestina kwa ajili ya kuwahudumia na kuwalea watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) hatua itakayosaidia watoto hao kuhifadhiwa na kupewa huduma.

Msadaa una thamani ya zaidi Sh.milioni 4.5 umetolewa na taasisi hiyo akishirikiana na wadau wa Element Club Msanii Gnako, Sheta ambao wamekuwa bega kwa bega na Doris katika jitahada hizo za wakusaidia watoto njiti.

Msaada wa vifaa utasaidia kupunguza hali ya kuwasafirisha watoto kwa njiti kutoka na machine tulioitoa inauwezo wa kusaidia watoto wawili kwa siku kwa ajili ya matibabu kwa kuwa watakuwa na vifaa vyao.

Akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa kwa vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation Doris Mollel amesema anamshukuru Mungu kwa kuumpa kibali cha kuwahangaikia watoto  waliozaliwa kabla ya wakati ili nao waweze kuishi kama watu wengine.

"Najua kazi hii ni ya Serikali kupitla Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lakini sisi wadau ambao tuko katika mashirika yasiyo ya kiserikali tunafanya kazi kupitia miongozo yao na tunafurahi kuwa hapa kuchangia vifaa hivi kwa ajili ya watoto Njiti na wamama ambavyo vitaleta auheni kwa watoto hao,"

"Nipende kuwashukuru Element, wasanii Gnako, Shetta na Dully kuweza  kushiriki kwenye usiku wa kusaidia watoto njiti na mama kwa usiku mmoja na kujipatia mapato ya kusaidia watoto jiti, sio mwanzo nasio mwisho litakuwa jambo endelevu kwa kila mwaka tutaacha alama ya vifaa"amesema Mollel.

Kwa upande wake Meneja Masoko na Mbunifu wa Elements Club, Maribeth Vuhahulla maarufu kama 'Lady Hahaa' amesema Elements imechangia  msaada huo amesema wameamua kuwasaidia watoto hao ili kupunguza vifo vinavyotokana na kukosa mahitaji mahimu katika malezi na matibabu huku akiwashauri wadau wengine kuunga juhudi hizo.

"Tumetoa msaada huo lakini sio mwisho tutaendelea kuchangia na pia tunawashukuru wasanii Gnako, Shetta kwa kuweza kutoa ushirikiano kwa kuweza kutoa burudani kupata mapato ya kusaidia mama wanaojifungua watoto njiti."amesema Lady Hahaa

Naye Msanii G Nako amesema kuwa hii ndio njia mojawapo ya kurudisha kwa jamii tunachokipata pia ni sehemu ya kuisadia Serikali kuboresha huduma za afya,, na kusaidia mashabiki wetu" amesema Gnako.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu  Mfawidhi wa Hospital ya Sinza Dk. Leonard Lutha, ameshukuru kwa msaada huo wa kusaidia wamama wanaoza watoto njiti tunashukuru, wanaozaliwa hospitalini hapo kwa mwezi nusu yao ni watoto njiti hivyo changamoto ya kuwalea ipo na uhitaji wa vifaa tiba ni mkubwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d066ae9186a2efb178af49f10cecdb32.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Na Brighiter Masaki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi