MSANII wa Vichekesho na Mchungaji wa 'Free Church' Emmanuel Mgaya, 'Masanja' amesema wazi kuwa wa Mtumishi wa Mungu anachaguliwa na Mungu so mwanadamu.
Akizungumza na waumini katika ufunguzi wa ibada ya Kanisa la 'Love Church' la Emmanuel Mathias, Mc Pilipili, Masanja amesema wanaomsema Mchungaji Pilipili hawamjui hana njaa.
"Mchungaji njaa anajulikana wanaosema kaanzisha Manisa anatafuta pesa Mc Pilipili hana njaa amefungua kanisa kuhudumia waumini nasio kutafuta pesa anazo za kutosha."
"Kama umaarufu anao pesa ametafuta kwenye kazi za Ushehereshaji nasio kwenye uchungaji hapa anachapa injiri kwa kwenda mbele wanaosema anafata pesa wazilete tuhudumie kwenye uhitaji." amesema Masanja
Aidha ameongeza kama uchungaji unalipa basi nawao wafungue, Mama Uchungaji anatumia IPhone macho matatu kuna shida hapo wameamua kuhudumia watanzania.