loader
Wanamitindo Zanzibar waahidi kuongeza pato la Taifa

Wanamitindo Zanzibar waahidi kuongeza pato la Taifa

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ya jukwaa la Mavazi ya Kiasili kusaidia Serikali ya Zanzibar kutangaza Utalii na kukuza pato la Taifa.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Julai 29 hadi 30 mwaka huu katika ukumbi wa front ocean Visiwani Zanzibar."

Akizungumza na Habari Leo, Mbunifu Mkongwe kutoka Visiwani Zanzibar ambae pia ni Muasisi wa jukwaa la ubunifu (Zanzibar fashion island) Waiz Shelukindo,  amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi julai mwaka huu likiwa na lengo la kutangaza utalii visiwani na Mavazi ya Kiasili.

"Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi lazima ikue hivyo lazima kuwepo Kwa Matamasha ambayo yanakumbusha na Kuonyesha vitu vipya hivyo tumeamua kutangaza utalii kwenye jukwaa la ubunifu wa Mavazi linalotarajiwa kufanyika julai 29 Hadi 30 mwaka huu katika ukumbi wa front ocean Visiwani Zanzibar."

Aidha ameeleza kuwa jukwaa hilo litakuwa la wazi Ili kuwapa fursa watu kuhudhuria Kwa wingi na kuona Kwa jinsi gani Kuna baadhi ya Mavazi ya Kiasili na kitamaduni hayapewi nafasi Kwa Sasa kutokana na utandawazi na tamaduni za kizungu.

"Kuna baadhi ya Mavazi mara nyingi yamekua hayaonekani lakini wabunifu kutokana na kazi zao wamekuwa wakitengeneza hivyo jukwaa hilo litaweza kuwapa fursa wabunifu kuonyesha Mavazi hayo."

Aidha Waiz amesema kupitia jukwaa hilo litashirikisha wabunifu wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Visiwa vya Comoro,Kenya, Uganda na nchi zingine nyingi Visiwani Zanzibar.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ae17e008176de992279b02c103751937.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Na Brighiter Masaki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi