loader
Kuweni makini kutafuta ushauri mitandaoni

Kuweni makini kutafuta ushauri mitandaoni

KATIKA siku za karibuni kumekuwa na tabia ya wanawake kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuelezea mambo kadhaa yanayowakabili katika maisha yao hususani ndani ya ndoa zao.

Katika mitandao hiyo wanawake wanaandika masuala ya maisha, namna anavyoishi na waume zao au malezi na mambo mengine mbalimbali ikiwa hata magonjwa yanayomkabili mmoja wa wanafamilia.

Katika kuomba ushauri, wapo wanaofikia kuwapiga picha wagonjwa au wakiwemo watoto au wengine ambao hawajiwezi kwa lengo la kuomba ushauri katika mitandao.

Ni dhahiri kuwa, iwapo mitandao hiyo itatumika vizuri inaweza kusaidia kukabiliana na changamoto za maisha lakini ni vema kuwa waangalifu kwa jambo unaloomba ushauri na pia kuchambua kwa undani kuhusu ushauri unaotolewa.

Ikiwa ni masuala ya magonjwa ni vema kuelezea ugonjwa unaosumbua kisha kutafuta daktari mzuri anayeweza kusaidia na si kutaka ushauri wa dawa ya kutumia kwani hakika si dawa iliyomponya fulani na wewe ikawa tiba.

Lakini ni vema kuzingatia, mila, desturi na tamaduni za Kiafrika na Kitanzania kwa ujumla huku ukimtanguliza Mungu mbele kwa kutumia imani yako katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokukabili na kamwe usikubali kutumia ushauri ambao kwa namna nyingine unaweza kukutumbukiza katika shida kubwa zaidi ya uliyonayo.

Hivyo ni vema kuwa waangalifu katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwani haiwezi kuwa suluhisho la changamoto na matatizo ambayo mtu binafsi au jamii inayotuzunguka.

Kwani kabla mitandao hiyo haijaingia nchini, masuala kama hayo yalikuwepo na njia mahususi zilitumika kupata ufumbuzi na siyo kufikia muafaka wa utatuzi wa changamoto kwa ushauri katika mitandao pekee.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7d69da16c57435f6e0ac6b8d20db7e20.PNG

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi