loader
Kichwa cha kwanza cha SGR chatua Dar

Kichwa cha kwanza cha SGR chatua Dar

KICHWA cha kwanza cha treni ya Reli ya Kisasa (SGR) cha Mkandarasi Yepi Markezi kwa ajili ya majaribio ya umeme katika kipande cha reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, kimewasili nchini juzi.

Kichwa hicho kina uwezo wa kwenda kwa kasi ya Kilometa 160 kwa saa, ambacho kitasaidia majaribio ya njia kwa mwendokasi uliozingatiwa katika ujenzi.

Kimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam wakati ujenzi wa SGR Dar es Salaam hadi Morogoro umefika zaidi ya asilimia 95 na kinatarajiwa kuanza majaribio hivi karibuni.

Akizungumzia ujio wa kichwa hicho Dar es Salaam jana, Naibu Meneja Mkuu wa Yepi Markezi, Erhan Cengiz  alisema kichwa hicho kitaendeshwa kwa umeme, kitatumika pia katika majaribio ya mifumo ya ishara.

“Mradi wa SGR ni ujenzi wa kisasa wa teknolojia ya kisasa ya hali ya juu, tunaweza kusema hii ni ya kwanza ya aina yake Afrika. Tunatarajia mwendokasi ya juu kuwa kilometa 160 kwa saa na tutatumia mifumo zaidi ya ishara kuwasiliana,”alisema Cengiz.

Aliongeza, “Sasa tunatarajia hatua ya kwanza ya majaribio ya kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kwa hiyo hili linahitaji vichwa maalumu vya treni ya kisasa ili tuweze kufikia viwango vinavyohitajika katika majaribio na kichwa kilichowasili kina uwezo huo.”

Alisema kichwa hicho kitatumia mifumo ya umeme ambayo wamekwishaiandaa katika ujenzi wa vipande vyote.

“Mara zote tunasema kuwa tunatekeleza mradi wa mfano kwa ushirikiano wa karibu na TRC chini ya usimamizi wa Rais Samia Suluhu Hassan na ujenzi unaendelea vizuri na haraka kama kila mmoja anavyoona,” alisema.

Ujenzi huo wa kilometa 300 kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umejengwa kwa gharama ya Sh trilioni 2.7, utafufua, itaimarisha, kuchagiza uchumi na maisha ya Mtanzania mmojammoja na ni treni ya kisasa na ya kasi kuliko zote ukanda wa Afrika.

Ujenzi huo unaofanywa na kampuni ya Uturuki ulianza Mei mwaka 2017 na ulisainiwa Februari 3, 2017.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5296cb37856694886e3003b3d40a1064.JPG

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi