loader
Bunge lapitisha muswada Umoja wa Wanawake EAC

Bunge lapitisha muswada Umoja wa Wanawake EAC

BUNGE la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limepitisha muswada wa kuundwa kwa Umoja wa Wanawake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mmoja wa wabunge wa bunge hilo kutoka Rwanda, Fatuma Ndangiza ambaye ni Katibu wa umoja huo, alisema umoja huo ni wa kwanza kuundwa tangu kuanzishwa kwa Bunge la Nne la EALA mwaka 2017.

“Tukiwa tunaadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani (leo) nchi za EAC zimepiga hatua kubwa kwa kupitisha kwa pamoja muswada wa kuundwa umoja wa wanawake ndani ya jumuiya utakaozingatia usawa wa mwanamke japo changamoto bado ni kubwa,” alisema Fatuma.

Msemaji wa umoja huo, Pamela Maasay, alisema umoja huo unalenga kuhamasisha mtangamano ndani ya EAC hasa namna ya kushirikisha wanawake katika uamuzi.

Alisema ndani ya EAC wanawake wana mchango mkubwa katika nyanja za kiuchumi, lakini bado kuna unyanyapaa na uonevu katika utoaji wa nafasi za uongozi.

Mbunge Abdullah Makame alipongeza uamuzi wa bunge hilo kukubali kupitisha hoja ya kuunda Umoja wa Wanawake wa EAC kwa kuwa miongoni mwa malengo ya EAC ni kuongeza usawa kwa wanawake katika jumuiya.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi