loader
Hongera Balozi Kazungu kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya

Hongera Balozi Kazungu kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya

BALOZI wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, anamaliza muda wake wa utumishi akiwa ametoa mchango mkubwa kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na Tanzania. Kazungu aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais John Magufuli Ikulu Dar es Salaam, Julai 30, 2018 kuwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania.

Tunampongeza Kazungu tukimtakia heri huku tukiungana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula kumhimiza kuendelea kuwa balozi bora wa kuitangaza vizuri Tanzania anaporudi nchini kwake.

Tunasema hayo tukifarijika kwa maneno aliyoyasema alipokutana na Waziri Mulamula hivi karibuni Dar es Salaam kuwa, amejifunza mengi mazuri kutoka Tanzania ukiwamo ukarimu na upendo wa Watanzania.

Ndio maana tunasema, kutokana na mema aliyoyaona na kuyaishi kutoka kwa Watanzania, popote aendapo ndani au nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kazungu awe balozi mwema kwa kutangaza sifa nzuri za Tanzania, vivutio na mazingira mazuri ya kikazi, kibiashara, uwekezaji, huduma na ukarimu vilivyopo Tanzania. Kimsingi, yapo mambo mengi makubwa na mazuri aliyoyafanya Balozi Kazungu akiiwakilisha Kenya nchini Tanzania.

Mawili kati ya mengi aliyoyafanya katika kuimarisha uhusiano wa nchi hizi za EAC ni pamoja na namna alivyochangia, kushiriki na hata kufikia mafanikio kwa ushiriki wake na wadau wengine katika juhudi za kuondoa vikwazo vya biashara baina ya Tanzania na Kenya, hali iliyoimarisha uhusiano, biashara na uchumi miongoni mwa nchi hizi.

Katika kipindi chake cha uwakilishi nchini Tanzania, Kazungu aliwasilisha waraka muhimu wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliomwandikia aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kuelezea kughadhabishwa kwa Serikali ya Kenya dhidi ya matamshi yaliyokuwa yametolewa na Mbunge wa Starehe, Charles Kanyi maarufu Jaguar.

Jaguar alikuwa ametoa matamshi yanayowataka raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wanaofanya shughuli za kibiashara nchini Kenya wakiwemo Watanzania, kuondoka ndani ya saa 24, hali iliyozua sintofahamu na mjadala.

Akiwasilisha waraka huo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Kazungu alisema msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta ni kuwapokea na kuwakubali ndugu zao wote wanaotoka nchi za EAC walioamua kuishi au kufanya biashara nchini Kenya.

Ndio maana tunakumbuka hayo huku tukisema, utendaj wa Kazungu umechangia kuziwezesha Tanzania na Kenya kuimarisha uhusiano wa kindugu, kijirani na kijamii na hapa anastahili pongezi kwani kazi yake imechangia kuchochea ukuaji wa biashara, uwekezaji na hata ustawi wa jamii katika nchi hizi mbili.

Ndio maana tunasema, hata mabalozi wa nchi nyingine, waendelee kuwa viungo bora wa uhusiano baina ya Tanzania na nchi zao kama Balozi Kazungu alivyochangia kuimarisha uhusiano bora baina ya Tanzania na Kenya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9b9fd9f14f690911270b94d6ee81fc9c.PNG

JUMATATU Mei 09, mwaka huu, lilifunguliwa Kongamano ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi