loader
Siku ya Wanawake: Mashirika ya himiza nguvu kwenye usawa wa kifedha

Siku ya Wanawake: Mashirika ya himiza nguvu kwenye usawa wa kifedha

NCHINI Tanzania, kama nchi nyingine nyingi barani Afrika, ingawa kuna sera na mfumo madhubuti wa kisheria wa kushughulikia ukosefu wa usawa wa kijinsia, kiutendaji, kanuni za kimila bado zinawabagua wanawake na kusababisha ubaguzi wa kifedha.

Kanuni za kitamaduni zinapunguza umiliki wa mali kwa wanawake na udhibiti wa rasilimali za kifedha,” alisema bwana. Hebu fikiria ulimwengu usio na ubaguzi wala upendeleo.

Ulimwengu wenye usawa na unaojumuisha watu wote. Ulimwengu ambao utofauti unathaminiwa na kusherehekewa. Kwa pamoja tunaweza kujenga usawa kwa wanawake. Kwa pamoja tunaweza #KuvunjaUbia. Hii ndiyo kaulimbiu ya Siku ya Wanawake mwaka huu.

Huadhimishwa kila Machi 8, Siku ya Kimataifa ya Wanawake ni maadhimisho ya kimataifa ya kukumbuka mafanikio ya kitamaduni, kisiasa, na kijamii na kiuchumi ya wanawake na inazingatia masuala kama vile usawa wa kijinsia, haki za uzazi, unyanyasaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake. Nchini Tanzania, siku hii ina umuhimu wa pekee hasa katika usawa wa kifedha.

Kwa mujibu wa taasisi ya kifedha ya Financial Sector Deepening Tanzania (FSDT); "Wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya watu na nguvu kazi nchini Tanzania na ni zaidi ya nusu (54%) ya wafanyabiashara wadogo nchini, lakini mchango wao katika shughuli za kiuchumi na ustawi wa kifedha uko chini sana." "…tumekaribia maono yetu makubwa ya kuwa kampuni ya kuimarisha usawa wa kijinsia.

Lengo letu kuu ni kupinga dhana potofu na kutoa fursa zaidi kwa wanawake ili kuongeza usawa kifedha," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa QNET Malou Caluza, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni hio katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.

“Ni wazi kuwa wanawake ni wahusika muhimu katika uchumi wenye afya na ustawi na biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa ajira hususan kwa wanawake,” aliendelea kusema mkurugenzi huyo. “Kuwa kampuni yenye usawa wa kijinsia itasaidia kuongeza mamilioni ya kifedha kwenye pato la taifa," alisema.

Uuzaji wa moja kwa moja ni njia ya mauzo inayotumiwa na makampuni mengi kutangaza bidhaa zao moja kwa moja kwa watumiaji wa mwisho kwa kufanya maonyesho madogo madogo ya bidhaa mbali mbali.

Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, anaelezea kuwa biashara ya mfumo huu ni mkombozi kwa wanawake hasa kwaajili inahitaji mtaji mdogo kuanzisha, swala ambalo linawakwamisha wanawake wengi.

"Kupitia mfumo huu, wanawake wanaweza kuruka vikwazo kama vile ukosefu wa mtaji, na kwavile mfumo huu ni wakujiajiri unawapa fursa kujipangia ratiba za kufanya kazi kulingana na mahitaji ya maisha yao ya kila siku," alisema katika taarifa hio. Akiendelea kusifia uongezeko wa wanawake wajasiria mali, alisema kuna fursa kubwa ya kujiajiri hususan kwa kutumia mifumo ya kidijitali.

"Wanawake wanaweza kujiajiri kwa kutumia miundombinu ya biashara za kidijitali ili kutoa fursa mpya za mapato na uuzaji wa moja kwa moja ni mfano mzuri wa fursa za kidijitali," alisema.

 "…mfumo huu wa biashara ni jukwaa ambalo wanawake wanaweza kuchukua mamlaka na kubadilisha maisha yao na hasa kipindi hiki cha kusherehekea mafanikio ya kiuchumi kwa wanawake."

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/83feb7d6fbc84f4872ab0fd01731a44d.jpg

OPERESHENI ya kuondoa wazururaji na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi