loader
Tuunge mkono juhudi za kuinusuru Ngorongoro

Tuunge mkono juhudi za kuinusuru Ngorongoro

JANA Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17, mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Aidha, akipokea majina hayo wazee wa kimila wa Maasai, Malaigwanak walikula kiapo kuilinda Hifadhi ya Ngorongoro kwa maslahi ya taifa.

Kwanza tunapongeza juhudi za serikali za kutekeleza agizo la Rais Samia la kuona namna bora ya kuendelea kuitunza tunu hii adhimu ambayo dunia nzima inaiangalia.

Aidha, tunawapongeza wananchi ambao wamepokea somo, wakalielewa na kuanza kuchukua hatua kwani kwa hatua zao wanasaidia kwa namna fulani kuwapo na ratibu nzuri ya wananchi walioamua kulinda hifadhi hiyo kwa manufaa ya taifa na dunia.

Ni kweli hatua zinazochukuliwa na serikali zinaonesha kujali maslahi ya taifa, wananchi na dunia kwa ujumla hasa ukiangalia historia ya mbuga hiyo ambayo haikuwa na tatizo miaka 60 iliyopita.

Ni kweli kuwa zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30 lakini leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo na kuifanya hifadhi hiyo kuanza kuwa na kitu si sawasawa.

Kuanza kuondoka kwa watu ndani ya mbuga hiyo tunaamini kabisa kutaambatana na kuondolewa kwa makazi ya binadamu yaliyozidi ambayo hayaleti sura nzuri ya uhifadhi katika eneo hilo muhimu kiikolojia na kwa historia ya binadamu.

Ni dhahiri hatua ya serikali ya kutenga eneo la kilometa za mraba 400,000 wilayani Handeni kwa ajili ya watu wanaoondoka katika hifadhi hiyo ni namna bora ya busara kabisa ya kuondoa migongano ya kimaslahi ambayo yataharibu utaratibu wa hifadhi hiyo muhimu inayotegemewa na hifadhi nyingine nchini na nchi jirani.

Ni matumaini yetu kwamba kauli ya viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote, itatekelezwa kwa busara kubwa ili hadhi ya hifadhi hiyo na nyingine kurejea kama zamani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/10ef5a3385cd6e9da4eb2e4e19d6b68a.PNG

JUMATATU Mei 09, mwaka huu, lilifunguliwa Kongamano ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi