loader
Wanawake msijiue kwa kuweka vitu sehemu za siri kufurahisha wanaume

Wanawake msijiue kwa kuweka vitu sehemu za siri kufurahisha wanaume

WANAWAKE wamekuwa wakitumia njia mbalimbali lengo tu wanaume wawapende wakati wote na wanafundishwa katika baadhi ya jamii wakiwemo wanawake na wasichana wanaoolewa.

Yapo mambo ya mila na desturi za Kitanzania, mwanamke anamfanyia mume wake kama ishara ya upendo na siyo kulazimisha kupendwa kwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuhatarisha afya.

Kutokana na kuongezeka kwa walimu katika masuala ya mahusiano kwa kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali ambazo wanawake wamekuwa wakikabiliana nazo, imefikia hatua baadhi ya wanawake kutojali uhai wao ili mradi amfurahishe mwanaume ambaye hata hivyo hatakuwa naye peke yake. Katika hilo, kuna mitandao ya kijamii inayomilikiwa na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wanawake na kuwauzia baadhi ya vitu vya kuweka sehemu za siri kwa lengo la kumridhisha mwanaume na kupata mwitikio mkubwa wa wasichana na wanawake.

Lakini sasa wataalamu wa afya wametoa tahadhari kwa wale wanaodanganyika kwa kuweka dawa za kuongeza hamu ya ngono ambazo hazijapimwa na wataalamu. Wanabainisha wanaofanya hivyo wako katika hatari kubwa kupata saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi nchini.

Mtaalamu na Mshauri Mwandamizi mwenye uzoefu wa Afya ya Umma, Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Dk Katanta Simwanza anasema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 kutoka katika kituo cha Saratani Ocean Road, aina ya magonjwa ya saratani yanayowapata wanawake wengi ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi (asilimia 43), saratani ya matiti (asilimia 14.2) na saratani ya koo (asilimia 3.8).

Anaeleza kuwa utumiaji wa dawa za kusisimua mwili ambazo hazijapimwa, ngono zisizo salama, kushiriki tendo la ndoa mapema na kujamiiana na wanaume wasiotahiriwa ni changamoto kubwa. Anasema kitendo cha kuondolewa kwa harufu ya asili ukeni kunasababisha maambukizi ya njia ya uzazi na kuongeza hatari ya unyanyasaji wa kijinsia.

Kutokana na kauli hiyo ni dhahiri kuwa mwanaume akikupenda hana sababu ya kutaka ufanye mambo hayo ambayo yataondoa asili ya mwanamke. Ni vema wanawake kujikubali jinsi walivyo na kamwe wasikubali kushabikia kila linaloandikwa katika mitandao ya kijamii kwani ni hatari kwa afya ikiwemo suala la kuweka vitu vya aina mbalimbali katika sehemu za siri.

Sio jambo jema kujidhuru mwenyewe kwa kumfurahisha mwingine, hivyo wanawake na watoto wa kike kuanzia sasa tambueni kuwa kufanya vitendo hivyo ni kujiweka hatarini na kupata ugonjwa wa saratani.

Ni vema kusikiliza wataalamu wa afya nchini katika masuala ya afya na siyo kufanya lile unalolipata kwa walimu mitandaoni na mwisho wake ni kifo na utamuacha huyo mwanaume unayetaka kumridhisha na afya yake njema na kupata mwanamke mwingine mwenye afya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cae19f023db63a64088a47e3109f4da7.PNG

NIPO nyumbani kwa Baba na Mama Chichi. ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi