loader
Simba: waje tu Pirates

Simba: waje tu Pirates

KIKOSI cha wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba, kinaendelea na maandalizi yake kuikabili Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwenye robo fainali za michuano hiyo na tayari kimeingia kambini mapema jana.

Mechi hiyo inayosubiriwa na wengi inatarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu, alisema maandalizi yao yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kujiandaa na mchezo huo huku lengo lao likiwa ni kushinda kwa idadi kubwa ya mabao.

Simba itaanzia nyumbani  na baada ya hapo itasafiri kwenda Afrika Kusini kurudiana na wapinzani wao Aprili 24 na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya nusu fainali.

“Maandalizi yetu yanaendelea vizuri kila kitu kinakwenda kama tulivyo panga malengo yetu ni kuhakikisha tunamaliza kazi kwenye mchezo wa kwanza ambao tutacheza nyumbani, wachezaji wetu wote ambao wanahusika kwenye mchezo huo wapo fiti na wanausubiri kwa hamu mchezo huo,” alisema Rweyemamu.

Kwa upande wake Meneja wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ameendelea na hamasa maalumu ambapo tangu juzi amekuwa akitembelea sehemu mbalimbali za Dar es Salaam akiambatana na baadhi ya viongozi wa sasa na wazamani kuhamasisha mashabiki wao kujitokeza kwa wingi siku ya mechi.

Ahmed alifanya uzinduzi  huo juzi Chang’ombe na jana alikuwa Kigamboni ambapo kundi la mashabiki wakimfuata kununua tiketi.

Shamra shamra zilianzia kwenye kivuko cha Pantoni mpaka Kigamboni na kurudi katika Soko la Samaki Feri ambapo vikundi mbalimbali vya ngoma vilikuwa vikitumbuiza mwanzo mwisho.

Ahmed amewasisitiza mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani baada ya kuruhusiwa kuujaza na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), alisema  mchezo wa Jumapili ni muhimu  kupata ushindi mnono kwa sababu wamedhamiria kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, hivyo ni vizuri wakamaliza kazi nyumbani.

“Wanasimba wenzangu Jumapili hakuna kazi nyingine zaidi ya kujitokeza uwanjani kuipa sapoti timu ili kufanikisha lengo la kutinga nusu fainali. Wakina Kapombe (Shomari), Kagere (Meddie), Bwalya (Rally)  peke yao hawatoshi bila sapoti yenu,” alisema Ahmed.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0384e02981b2a44b19e219147aea2c88.jpg

VINARA wa Ligi Kuu, Yanga SC, wanahitaji ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi