loader
Ndoa mpya ya Haji Manara gumzo

Ndoa mpya ya Haji Manara gumzo

 “HAIKUWA rahisi, lakini kila jambo lina utaratibu wake vile Muumba wetu alivyolijaalia,” hivyo ndivyo alivyoandika Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara katika ukurasa wake rasmi wa instagram na kuongeza kuwa:

“Thanks Baba na Mama yangu kwa barka zenu kwetu,,,na karibu mke wangu @rubynah_bnt_salum kwenye familia yetu.”

Baada ya chapisho hilo zilianza kusambaa picha mbalimbali zikimuonesha Haji akiwa na mkewe mpya na pongezi kumiminika.

Miongoni mwa watu wa mwanzo kupongeza kupitia ukurasa wake wa instagram ni msanii Wema Sepetu, aliyeandika: “Mashallah mke wetu ana haiba....hongera sana Haji wangu... Allah bariq ndoa yenu...

 “Hongera kaka,” ameandika Farid Mussa mchezaji wa Yanga.

“Neno moja la pongezi kwa Buggati,” Ali Kamwe mchambuzi wa soka.

“Ikawe kheri Insha’allah, hongera kaka yangu,” Zamaradi Mketema .

Makundi mbalimbali ya whatsapp hasa yale ya wanamichezo, suala la ndoa ya Haji limechukua nafasi tangu asubuhi leo, huku walio wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo.

Tofauti na ndoa yake ya Desemba mwaka 2020, alipomuoa Naheeda Abdallah,  iliyokuwa na mbwembwe, safari hii ndoa ya Haji imekuwa kimyakimya na wengi wala hawakujua imefungwa lini, hadi picha zilivyoanza kusambaa mitandaoni.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/537e053d5486c86439d1bda328109622.jpg

VINARA wa Ligi Kuu, Yanga SC, wanahitaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi