loader
The Brothers tamthilia yenye mengi ya kujifunza

The Brothers tamthilia yenye mengi ya kujifunza

THE Brothers ni miongoni mwa tamthilia bora za Kifilipino zilizojichukulia umaarufu duniani kutokana na ujumbe ulioko ndani yake.

Tamthilia hii ya kigeni ya Ufilipino imetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili hakika inavutia, inahuzunisha, inafundisha na kuburudisha hasa kwa watazamaji wanaoifuatilia kwenye chaneli ya ST Novela E inayopatikana kwenye king’amuzi cha StarTimes imeteka macho ya watazamaji wengi.

Kile ambacho kiko ndani ya tamthilia hiyo kwa maana ya stori inayogusa upande mmoja masuala ya maisha, mapenzi, uhalifu na namna mamlaka mbalimbali zinavyoshughulika na makosa kutafuta suluhu.

Tamthilia hizi za kigeni ni nzuri na zenye funzo kwa wasanii wa Tanzania, pengine wakitizama na wao wanaweza kupata kitu, au wazo linaloendana na tamaduni za nchi na wao kuja na stori zitakazovutia watazamaji hao.

Hadithi hii inahusu mapacha wawili, Dominador de Leon ‘Ador’ na Ricardo Dalisay  ‘Cardo’. Ador ni Ofisa wa Polisi wa kuigwa aliyejitolea kwa maadili ya huduma, heshima na haki.

Mapacha hao walitenganishwa kwa sababu za kifedha, hata kama walifuata njia ya kuwa maofisa wa polisi.

Maisha yao yanabadilika ghafla Ador anaposalitiwa na kuuawa na Joaquin, baada ya kufuatilia harambee ya mwanadada huyo ya kusafirisha watoto.

Kwa kutaka kuficha ukweli kwamba Ador anauawa akiwa katika harakati, Jenerali Delfin Borja, mjomba wa mama wa Cardo na Ador na Mkurugenzi wa Kitengo cha Kupambana na Uhalifu (CIDG), anamwamuru Cardo kuchukua utambulisho wa Ador na kuendeleza misheni aliyoiacha marehemu kaka yake

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2eb3d7b9eb1a48b0c41eb0f02f9c9e42.jpg

OPERESHENI ya kuondoa wazururaji na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi