loader
Nabi ataka usajili mpya Yanga

Nabi ataka usajili mpya Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema ili timu hiyo iweze kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa, wanalazimika kuongeza baadhi ya wachezaji kwenye nafasi za ushambuliaji na ulinzi.

Yanga inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, hivyo mwakani italiwakalisha taifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Nabi alisema ameifatilia kwa karibu mashindano hayo na amegundua yanahitaji timu yenye wachezaji wenye uzoefu na wapambanaji, hivyo lazima waingie sokoni ili kufanya usajili mzuri.

“Timu tuliyonayo msimu huu ni nzuri isipokuwa tunahitaji kwa malengo tuliyonayo kwenye michuano ya kimataifa lazima tuziboreshe baadhi ya sehemu ili kujenga kikosi cha ushindani kwa ajili ya michuano ya kimataifa,” alisema Nabi.

Kocha huyo alisema malengo yao ni kuongeza wachezaji watano, kati yao watatu wa kigeni na wawili wazawa na ana amini kikosi chake kitakuwa tayari kwa mapambano ya kuwania taji la Afrika.

Aidha, kocha huyo alisema maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo dhidi ya Namungo FC Aprili 23 yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema malengo yao ni kuchukua pointi tatu kwenye mchezo huo ili waende kwenye mchezo dhidi ya Simba wakiwa na pengo kubwa la pointi dhidi yao ambao wanashika nafasi ya pili.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f1b6a1c8ffbd0795bbdbaeae527b3e55.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi