loader
Ikulu, TRA, Tanesco zang’ara Mei Mosi

Ikulu, TRA, Tanesco zang’ara Mei Mosi

TIMU za michezo ya netiboli na soka za Ofisi ya Rais Ikulu, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), zimegawa dozi kwa timu ilizocheza nazo katika mashindano ya Kombe la Mei Mosi, yanayoendelea kwenye viwanja vya Jamhuri, Shell Complex, Kilimani na Mtelekezo jijini Dodoma.

Kwa upande wa netiboli timu ya Ikulu iliwafunga Benjamin Mkapa Hospital (BMH) kwa magoli 28-13. Washindi wenye kikosi kikongwe na chenye uzoefu mkubwa walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 13-6.

Nayo timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), iliwachabanga Wizara ya Kilimo kwa magoli 30-16. NCAA waliongoza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa magoli 17-7, nayo timu ya Kongwa DC, iliadhibiwa na Hazina kwa kufungwa magoli 31-9. Hazina walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 19-2.

Katika mchezo wa soka uliofanyika Uwanja wa Mtelekezo, mabingwa watetezi timu ya TANESCO waliwafunga Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa magoli 6-0.

Nao TRA waliwafunga Wizara ya Afya kwa magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kilimani. Magoli ya TRA yalifungwa na Himran Ntabudyo na Maxmilian Maguncho.

Katika michezo mingine ya netiboli Uchukuzi  waliwafunga Wizara ya Madini kwa magoli 43-9. Washindi waliongoza kipindi cha kwanza kwa magoli 22-5; nao Wizara ya Nishati waliwashinda Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa magoli 26-21.

Hadi mapumziko Nishati waliongoza kwa magoli 12-10; nao Mzinga waliona mwezi kwa kuwafunga Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa  magoli 33-16.

Nao Uchukuzi SC waliwafunga Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) kwa magoli 6-0 katika mchezo wa soka, nayo Wizara ya Nishati iliwafunga Watoto wao Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwa magoli 2-1.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2e3a0d6207c7a19f777f02b62bca4cf3.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi