loader
TCCIA wajipanga kutumia fursa ya biashara DRC

TCCIA wajipanga kutumia fursa ya biashara DRC

CHAMA cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Kigoma kimejipanga kukuza biashara kwa kutumia fursa ya uanachama wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DCR) kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Kigoma, Abdul Mwilima alisema jana kuwa, Ukanda wa Mashariki ya DRC una karibu watu milioni 30 ambao kwa kiasi kikubwa hakuna uzalishaji wa bidhaa za viwandani na kilimo, hivyo ununuzi wao hufanywa kupitia mkoa huo.

Alisema katika mazungumzo na viongozi wenzao wa Jimbo la Katanga (Lubumbashi), Kivu Kusini (Bukavu), Jimbo la Tanganyika (Kalemie) na Chemba ya Kivu Kaskazini (Goma), wanaamini kuingia kwa DRC katika EAC kuna fursa kubwa ya biashara na uwekezaji.

Alisema takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha hadi mwaka 2018 biashara yenye thamani ya Sh bilioni 750 ilifanyika kupitia Mkoa wa Kigoma. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma, Raymond Ndabhiyegetse alisema eneo la Mashariki ya DRC kwa maana ya Kalemie, Kivu na baadhi ya maeneo Bukabu na Lubumbashi yanategemea usafirishaji wa bidhaa kupitia Bandari ya Kigoma na sehemu kidogo ya Burundi na hivyo biashara kwa Mkoa wa Kigoma kwenda DRC ni kubwa.

Alisema baadhi ya maeneo ya Mashariki ya DRC hali ya amani si nzuri na hiyo inaongeza utegemezi wa bidhaa za kilimo na viwandani kwa wananchi na watu wa eneo hilo vikiwamo vyakula.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kufanyika kwa kongamano la biashara la mkoa huo ni moja ya malengo ya mkoa kukaa na viongozi na wafanyabiashara kuona namna wanavyoweza kufanyabiashara na uwekezaji kwa pamoja.

Alisema pamoja na kuzungumzia biashara na uwekezaji, pia suala la ulinzi na usalama litapewa nafasi kwenye mazungumzo hayo sambamba na vikwazo vinavyochangia kutofanyika vizuri kwa biashara za kuvuka mpaka.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kongamano hilo pia litajenga uhusiano na kuimarisha mawasiliano kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo ili wajenge uthubutu wa kutumia fursa iliyopo kwenye biashara ya kuvuka mpaka.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/75219b6e7bf0c366ee29a88f0f71b8bd.jpeg

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi