loader
Ukraine yatuhumu vikosi vya Urusi

Ukraine yatuhumu vikosi vya Urusi

UKRAINE imetuhumu vikosi vya Urusi kuhusika na wizi wa vifaa vya shambani vyenye thamani ya mamilioni ya dola na kuvisafirisha hadi Chechnya, mtandao wa CNN umeripoti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vifaa hivyo, vinavyojumuisha mashine 27 za kuvunia mazao na kuchanganya, vilichukuliwa kwa muuzaji John Deere katika Jiji la Melitopol na vilikuwa na thamani ya jumla ya dola milioni 5.

Ofisa wa kampuni hiyo aliiambia CNN kuwa kulikuwa na "makundi hasimu" ya wanajeshi wa Urusi wanaoiba mashine, na wengine wakija asubuhi na wengine jioni.

Vifaa vingine vilipelekwa katika kijiji cha karibu, lakini mashine zingine zilichukuliwa umbali wa maili 700 hadi Chechnya, ambapo inaonekana kuwa kwenye shamba nje ya Grozny, kulingana na wafuatiliaji wa GPS.

"Wakati walipochukua machine hizo  hadi Chechnya, walikuwa hawana hata uwezo wa kuziwasha kwa sababu zilikuwa zimefungwa kwenye mfumo ambao ulizimwa na kampuni,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3fae8e2cbdb5793560e5d220cf580aba.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: Kyiv, Ukraine

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi