Kampuni ya kutengeneza magari ya Ufaransa ya Renault inapanga kuuza hisa zake za Avtovaz ya Urusi kwa kiasi cha ruble 1, Wizara ya Biashara ya Urusi imetangaza.
Hata hivyo, Renault, imekataa kutoa maoni kuhusu mpango huo.
Wizara ilisema, Renault itahamisha hisa zake za asilimia 68 kwa taasisi ya utafiti wa magari ya NAMI Russia, inayojulikana kwa kubuni Seneti ya Aurus, gari la kwanza la kifahari nchini humo, ambalo kwa sasa linatumiwa na Rais Vladimir Putin.
Renault inaonekana ilichukua hatua hiyo kwa kushindwa kuimarisha shughuli zake za Urusi.
Wizara ya Biashara pia ilisema kiwanda cha Renault huko Moscow, ambacho huzalisha magari chini ya chapa ya Renault na Nissan, kitahamishiwa umiliki chini ya serikali ya jiji hilo.