loader
Matokeo Kagera yawatesa Azam

Matokeo Kagera yawatesa Azam

BEKI wa Azam, Bruce Kangwa ameeleza namna walivyosikitishwa na matokeo ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar jana licha ya kukiri mchezo huo ulikuwa mgumu zaidi kwao.

Azam imefungwa mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba ikiwa ni mechi ya tatu sasa mfululizo kwenye ligi bila ya matokeo. Kabla ya mechi hiyo, Azam ilifungwa na Yanga mabao 2-1 kabla ya sare ya 2-2 dhidi ya Geita Gold.

“Kwanza tunamshukuru Mungu tumemaliza salama mchezo huu, matokeo hayakuwa yale tuliyoyategemea kama wachezaji hasa kwa timu pia, ukiangalia kwa namna tunavyopambana kuhitaji matokeo, lakini ndiyo mpira na sasa tunaangalia mechi zinazokuja maana hii ishapita.

“Mechi zote zimekuwa ngumu kwa sasa na hii ndiyo ligi ilivyo ushindani kila timu zinapokuja kwetu, sasa tunajipanga, tutarudi Dar es Salaam kujipanga vizuri kwa mechi inayokuja kuona tunafanikisha kupata ushindi,” amesema Kangwa.

Azam sasa inajipanga kuumana na KMC Jumamosi hii, huku kukiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 2-1 walipokutana na timu hiyo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7994cb20ef03577719dadf26a4d98e96.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi