MASHINDANO ya kumtafuta Miss Tanzania yanatarajiwa kufanyika Mei 20, 2022 ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa mashindano hayo, Azma Mashango, amewaomba wananchi kujitokeza siku hiyo kushuhudia mashindano hayo.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mashindano hayo jana, ilihudhuriwa na Miss Tanzania mwaka 2020/21,Juliana Rugumisa, ambaye baadaye alinyang’anywa taji hilo na kupewa aliyeshika nafasi ya pili, Rosey Manfere.