loader
Shirika laboresha mazingira soko Buguruni

Shirika laboresha mazingira soko Buguruni

WAFANYABIASHARA wa soko la Buguruni wameishukuru serikali na mfadhili kwa kuboresha soko hilo huku wakiomba iendelee kufanya maboresho makubwa liwe soko la kimataifa.

Wafanyabiashara waliozungumza na HabariLEO sokoni hapo jana, wamempongeza mfadhili ambaye ni Shirika lisilo la kiserikali la ‘Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) waliojenga soko hilo kwa kubadilisha taswira ya awali na kulifanya kuwa bora kuliko lilivyokuwa awali.

“Naishukuru serikali kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala kwa kumkubalia mfadhili kutujengea soko ambalo sasa linakidhi matakwa yetu ya usalama hususani kipindi hiki cha masika,” alisema Juma Said.

Kwa upande wa mamalishe, walisema kuboreshwa kwa soko hilo kumewawezesha kuendesha shughuli zao katika mazingira safi na salama bila kuchanganyika na biashara nyingine tofauti na ilivyokuwa awali. “Kwa hali ilivyo sasa ni bora zaidi ya awali ambapo mazingira yetu ya mapishi hayakuwa rafiki kwa afya za binadamu, tulikuwa tunajitahidi hivyo hivyo ili tutoe huduma na sisi pia tupate riziki lakini kwa sasa tuna majiko ya kisasa yaliyounganishwa na gesi…GAIN wametupatia mtungi wa gesi kila mmoja na jiko lake,” alisema Sophia Abdallah.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wamelalamikia baadhi ya miundombinu ya soko hilo kutokuwa katika hali nzuri ikiwamo mitaro na barabara za kuingia sokoni hapo pamoja na chemba za vyoo katika soko hilo kuwa mbovu na kupendekeza zikarabatiwe. Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo, Mwenyekiti wa soko, Said Kondo alisema limeboreshwa katika jengo moja, choo, sehemu ya wachinjaji wa kuku na mamalishe lakini si miundombinu.

“Kuna kitu wafanyabiashara wetu wanachanganya. Maboresho ni kwenye sehemu ndogo na mfadhili, si mradi wa soko zima hivyo maeneo niliyokutajia ndiyo yaliyoboreshwa,” alisema Kondo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa soko, mfadhili hakushughulika na miundombinu kwani alifika kwa ajili ya mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara ili wakabiliane na mapambano dhidi ya Covid-19 na waliomba fedha hizo wazielekeze kwenye uboreshaji wa soko na bajeti yao iliishia katika maeneo hayo yaliyoboreshwa. Mkuu wa soko hilo, Ramadhan Mfinanga alisema maboresho ya soko hilo yamenufaisha wafanyabiashara 2,635.

Vizimba 276 vimejengwa katika soko hilo huku maboresho makubwa yakitarajiwa kufanywa na Halmashauri ya Jiji kwa kujenga barabara na mitaa ya soko kwa kiwango cha zege kuondoa kero iliyopo. Soko la Buguruni lipo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala lililojengwa mwaka 1978 huku likiwa miongoni mwa masoko makubwa yanayotegemewa mkoani Dar es Salaam.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/56c0db7d589e03e0d361e3d6046eae06.jpeg

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Na Dunstan Mhilu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi