loader
Tanzania mguu sawa Tuzo za AMVCA

Tanzania mguu sawa Tuzo za AMVCA

AFRICA Magic kwa kushirikiana na kampuni ya MultiChoice Africa, imetangaza rasmi msimu wa 8 wa tuzo za kimataifa za AMVCA zitakazofanyika Lagos, Nigeria, Mei 14 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera kwa washiriki wanaowania tuzo hizo kutoka Tanzania, Ofisa Uhusiano kutoka MultiChoice Tanzania, Grace Mgaya, amesema baada ya kusubiri kwa muda mrefu tuzo hizo zimerejea.

“Baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu hatimaye tuzo hizi zimerejea tena kwa kishindo na katika msimu huu  wa 8 Tanzania imefanikiwa kupeleka washiriki wawili.

"Tanzania itawakilishwa na Juma Sada, mtayarishaji wa filamu ya Ugonjwa wa Kifo sambamba na wawakilishi kutoka MultiChoice Tanzania,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja kitengo cha Utayarishaji Bodi ya Filamu Tanzania, Benson Mkenda amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za uzalishaji filamu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0d9105787400777c3cad3c2ba9ab94dd.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi