loader
Rais Samia ziarani Uganda

Rais Samia ziarani Uganda

RAIS  Samia Suluhu Hassan akiagana leo Mei 10, 2022  na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akielekea nchini Uganda kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Yowei Museveni.

Ziara hiyo ni ya leo na kesho ambapo inalenga kuimarisha na kudumisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu, Zuhura Yunus  imeeleza kuwa katika ziara hiyo, wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati, biashara, usafiri, maendeleo ya miundombinu pamoja na sekta za afya.

“Hii itakua ni ziara ya kwanza ya kiserikali nchini kufanywa na Rais Samia tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021” imeeleza taarifa hiyo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d1541dda3f1094ab7fc473c2645c45bb.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi