loader
China yaipa Muhimbili msaada wa vifaa tiba

China yaipa Muhimbili msaada wa vifaa tiba

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepokea vifaa tiba yenye thamani ya Sh milioni 139.7 kutoka kwa serikali ya China.

Akipokea msaada huo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MNH, Prof. Laurence Muser,  amesema vifaa hivyo vitatumika kwa wagonjwa mahututi na sehemu zingine.

Amesema wamekuwa na uhusiano mzuri wa ushirikiano, ambao umedumu kwa miaka 40 sasa.

"Kwa upande wa wataalamu wa afya tunashirikiana hata sasa kuna madaktari wa China wapo MOI na JKCI na hospitali zingine kama Musoma kule wapo na Mbeya pia.

"Wataalamu tunaowapata kutoka kwao ni kwa upande wa usingizi, wagonjwa mahututi na upasuaji wa watoto na wataalam hawa huwa wanakuja na wanakaa miaka miwili," ameeleza.

Prof Museru amebainisha kuwa kupitia ushirikiano huo serikali ya China ilitoa msaada kwa ajili ya jengo la MOI.

Kwa upande wake mwakilishi wa kikundi cha matibabu cha China Meng Yong, amesema hivi sasa madaktari 11 wapo nchini ambapo wawili wako MOI, wawili JKCI, wawili Mbeya na watano Muhimbili.

"Urafiki wetu ni wa muda mrefu kwa Muhimbili na kwa Tanzania nzima na timu yetu ya tiba wanafika hapa na wao huja kwetu kubadilishana uzoefu, hivyo tutaendeleza ushirikiano zaidi,"amesema Yong.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/defdd8fce8f3bdb3d91c7404f39a1b81.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi