loader
Daily News Digital watakiwa kujinafasi

Daily News Digital watakiwa kujinafasi

MITANDAO ya kijamii ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), imetakiwa kujitangaza na kuongeza ubunifu, ili iwe ya kiushindani kwa kupata watazamaji na wafuatiliaji wengi zaidi wa mitandao hiyo.

Hayo yamesemwa na Wakurugenzi wa Bodi ya TSN, wakiongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Hab Mkwizu, walipotembea chumba cha habari cha mitandao hiyo, Barabara ya Samora, Dar es Salaam leo.

“Mnatengeneza maudhui mazuri, lakini hatuyaoni kwa vile hamjitangazi, wapo watumishi wa umma na viongozi wa serikali hawaijui mitandao yenu, msijifungie itangazeni kwa nguvu zote, tunapoingia huko kwenye makundi ya whatsapp basi tukutane na link au habari kutoka Dailynews Digital,” amesema Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Mitandao ya kijamii inayomilikiwa na TSN ni Daily News Digital, Daily News/ HabariLeo Istagram, Twitter na Youtube channel.

“Makatibu wakuu wa taasisi na idara za serikali, wakuu wa mashirika, wabunge ni watu wenu hao hakikisheni wanawafuatilia, fanyeni matangazo kwa nguvu,” amesisitiza.

Kwa upande wa mjumbe wa bodi hiyo, Titus Kaguo amesisitiza kufanyika matangazo kwa wingi na kuwataka watumishi wa TSN kuacha kuweka ‘status’ za Simba na Yanga, badala yake waweke kazi zinazofanywa na Daily News Digital, ili kujitangaza.

Kwa upande wa mjumbe mwingine wa bodi ya TSN, Habibu Suluo alishauri uongozi wa TSN kutoa nafasi kwenye magazeti yake, upande wa mbele na kutangaza mitandao yake ya kijamii.

Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Hab Mkwizu ambaye aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 21, mwaka jana.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Titus Kaguo ambaye ni Meneja Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, Erasmus Uisso na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Teddy Njau.

Wengine ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), Habibu Suluo, Mhadhiri Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania, Dar es Salaam, Dk Julius Lugaziya na Meneja Kampuni ya Ujenzi na Ushauri katika Masuala ya Ujenzi ya Africa Consulting Limited ya Mpanda, Katavi, Andrew Gewe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/32da5b689c1fee7b0014c489c1cbb484.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi