loader
Mwamnyeto awapa neno wenzake

Mwamnyeto awapa neno wenzake

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amewataka wachezaji wenzake kuongeza mapambano ili kutimiza lengo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na HabariLEO, nahodha huyo alisema matokeo ya sare katika michezo mitatu iliyopita isiwavunje moyo bado wanapaswa kuongeza juhudi katika kila mechi zilizobaki ili kurudi kwenye mwenendo wao walioanza nao msimu huu.

“Inawezekana ni uchovu sababu hivi karibuni tumecheza mfululizo, lakini hiyo haipaswi kuwa sababu ya msingi itakayotufanya kupoteza ubingwa kitu cha msingi ni sisi wachezaji tuongeze juhudi kwenye mechi zetu zilizobaki ili kutimiza malengo ambayo ni ubingwa,” alisema Mwamnyeto.

Nahodha huyo ambaye yupo katika harakati za kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, alisema kwa sasa kila mchezaji amepewa majukumu yake ya kufanya na anamiini kwakutimiza hilo litasaidia kuhakikisha walichokikusudia wanakitimiza.

Mchezaji huyo alisema pamoja na presha kuwa kubwa kwao lakini kwa ubora wa kikosi chao bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi hizo saba zilizo salia ispokuwa kitu cha msingi ni wao kutimiza malengo yao na mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti.

Mwamnyeto alisema Yanga ni timu kubwa na msimu huu umekuwa na mafanikio makubwa kwao, hivyo haitapendeza kama watalikosa taji hilo ndio maana yeye akiwa kama kiongozi wa wachezaji amewaomba wenzake kuendeleza kasi waliyoanza nayo msimu huu.

Mwishoni mwa wiki hii Yanga itakuwa ugenini Uwanja wa Jamhuri Dodoma kucheza na Dodoma Jiji FC, mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na ubora waliokuwa nao wenyeji wa mchezo huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b45b64384902c93cb378e30cafb2b000.jpg

VINARA wa Ligi Kuu, Yanga SC, wanahitaji ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi