WATU 4,000 wamenufaika na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu ( THRDC) katika kipindi cha miaka 10.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa Mei 13,2022 na Mkurugenzi wa THRDC, Onesmo Olengurumwa katika maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao huo, ambao amesema watu hao wamewatetea mahakamani na maeneo mengine ya haki za binadamu.
Amesema pia wameshiriki katika mabadiliko mbalimbali ya sheria ikiwemo sheria ya vyombo vya habari.
"Katika kipindi cha miaka 10, jumla ya sheria 25 tumeshiriki kuzifanyia marekebisho, ikiwemo sheria ya takwimu ya mwaka 2015," amesema Olengurumwa
Pia Mkurugenzi huyo amesema serikali imeonesha utayari kufanyiwa maboresho ya sheria za vyombo vya habari.