loader
Musoma watumia Sh Mil. 100  makundi  kiuchumi

Musoma watumia Sh Mil. 100 makundi kiuchumi

HALMASHAURI ya Manispaa ya Musoma, imetumia jumla ya Sh Milioni 100 kutoka kwenye mapato yake ya ndani, kutekeleza mpango wa serikali kuinua kiuchumi wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Jacqueline Wanzagi, amesema hayo leo Mei  13, 2022 kwenye uzinduzi wa Wiki ya Ubunifu, ambayo kimkoa imefanyika katika manispaa hiyo.

Amesema kiasi hicho kimetolewa katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Machi 2022 kwa vikundi 17 na wenye ulemavu 11.

Kati ya vikundi hivyo, 10 ni vikundi vya wanawake, saba ni vikundi vya vijana, wakati kwa wenye ulemavu imetolewa kwa mtu mmoja mmoja.

Maadhimisho hayo ambayo kitaifa yalianza mwaka 2015, mkoani Mara yameanza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa kaulimbiu: "Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.”

Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Halfan Haule.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eabaad93564649f9350943813ae5efff.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Editha Majura, Musoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi