loader
Simba waachana na Morrison

Simba waachana na Morrison

KLABU ya Simba imempa mapumziko hadi mwisho wa msimu huu wa mwaka 2021/2022 kiungo mshambuliaji wake Bernard Morrison.

Taarifa kwa umma iliyotolewa muda mfupi uliopita na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez imesema Simba imefikia uamuzi huo, baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulika na mambo yake binafsi.

“Simba inamshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu yetu.

“Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kusaidia kupata mafanikio kadhaa, ikiwemo kucheza Robo Fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi,” imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa:

“Simba inamtakia kila la heri Bernard Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadaye.”

Msimu huu wa ligi unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi uja, ambapo mkataba wa Morrison aliyejiunga na Simba miaka miwili iliyopita akitokea Yanga ya Dar es Salaam utamalizika hivi karibuni.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ec50838dc93812a3db59b856aa836735.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi