loader
Rais Samia apongezwa utetezi haki za binadamu

Rais Samia apongezwa utetezi haki za binadamu

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujipambanua kuwa mtetezi wa haki za binadamu.

Makala ameyasema hayo leo Mei 13,2022 jijini Dar es Salaam  katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu na Nafasi za Kiraia Tanzania (THRDC).

" Wapo watu wanasema kwa maneno, lakini wewe unasema kutoka moyoni, toka serikali yako ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani ulisema unataka haki, tumeona uliposema hutaki kodi za dhuluma, ukataka kodi ikusanywe kwa haki, hiyo ilidhihirisha wazi kuwa unapenda haki.

"Arusha ulipokutana na waandishi wa habari ukasema sheria zote kandamizi wazilete zifanyiwe kazi, kwa sababu unapenda haki;...

"Kama Bosi wangu Rais ni mtetezi wa haki za binadamu na mimi nakaribisha asasi za kiraia ofisini kwangu, mje tufanye kazi," amesema.

Naye Mbunge wa viti maalum CCM Neema Lugangira ameitaka THRDC, kusimamia na kulinda  sheria na haki za watoto mitandaoni sambamba na wanawake viongozi, ambao mara kadhaa wameonekana wakidhalilishwa.

Naye Katibu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amewapongeza THRDC kuhakikisha wanasimama na kutetea haki za wanaharakati waliokuwa wakikamatwa katika nyakati mbalimbali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bd78a9358f281906eadd2f53ec92eb90.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi