loader
Wawekezaji wahakikishiwa raha Tanga

Wawekezaji wahakikishiwa raha Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima, amesema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, watafanya kila linalowezekana, ili mwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vilainishi na mafuta kwa ajili ya mashine na magari cha Mogas apate leseni.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho, baada ya kupata malalamiko ya kukwamishwa kwa mwekezaji huyo katika upatikanaji wa leseni.

“Nataka nimhakikishie mwekezaji Mogas, serikali itafanya kila linalowezekana, ili apate leseni na kila anachohitaji kifanyike ili uwekezaji uende mara mbili.

“Sasa hao wanaokuja wanatoa taswira kwa watu wengine kwamba Tanga ipo kwa ajili ya kupokea mitaji na uwekezaji na wanapeleka ujumbe mzuri kwa watu wengine na serikali ya mkoa tunawaunga mkono asilimia 100.

“Tanga nimeweka utaratibu wa kuhamasisha wawekezaji kushiriki na sisi moja kwa moja kwenye maendeleo ya serikali ya mkoa, kwa hiyo kama kuna mwekezaji amekuja ana jambo lake, urasimu umekuwa mwingi tunataka kuviondoa hivyo,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mogas, Geofrey Rugazoora, amesema wanaishukuru serikali mkoani Tanga, ambapo pia ameahidi kutoa mchango chanya katika kuchangia maendeleo mkoani hapa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/086a5c7f3d80c2feef0ab8f69e0edcbd.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Amina Omary, Tanga

1 Comments

  • avatar
    emmanuel
    13/05/2022

    Habar, maoni yangu ni kwamba; mnapoweka habar mjitahid kuandikwa pia wpi na lini tukio limetokea.ahsante

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi