loader
Chongolo atoa maagizo mbolea ya ruzuku

Chongolo atoa maagizo mbolea ya ruzuku

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametaka kuharakishwa kwa mpango wa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima nchini.

Ameyasema hayo leo Mei 13, 2022 wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha mbolea ya asili  cha  Itracom kilichopo eneo la Viwanda Nala jijini Dodoma, ambacho kinajengwa na mwekezaji kutoka Burundi.

Kiwanda hicho  ujenzi wake ulianza Julai, 2021 na kinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2022 ambapo kwa sasa kimefikia asilimia 80.

Kinatarajiwa kuanza uzalishaji wa awali Juni na Julai mwaka huu, huku kikitarajiwa kuzalisha zaidi ya ajira 3,000 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya  tani 600,000 za mbolea kwa mwaka baada ya kukamilika, ambapo katika hatua ya awali kitazalisha tani 200,000.

Chongolo ametoa maagizo hayo kwa Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Kilimo kuharakishwa mchakato wa upatikanaji wa ruzuku kwenye mbolea, ili kudhibiti upandaji wa bei inayowaumiza wakulima.

Amesema hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan, aligawa vitendea kazi kwa maofisa ugani na kutoa maelekezo mahsusi ya kutaka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Kilimo kukaa pamoja, ili kuhakikisha jambo hilo linatekelezeka.

Amesisitiza kuwa ruzuku hiyo inayokwenda kuwekwa katika mbolea ni lazima iwe yenye tija na yenye kulinda wawekezaji wa ndani ya nchi.

Pia amekemea baadhi ya taasisi na kampuni za serikali zinazohusika kusimamia mbolea kuacha kufanya kazi kwa mazoea, badala yake  zifanye kazi kwa ushindani kwa kuratibu na kusimamia bei ya mbolea.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/75de7b4f20d86eb8a5e8a1450050153f.jpg

MBUNGE wa Kigamboni, Dk Fausitine Ndugulile (CCM) ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi